15 February 2013

HUYU NDO MWANA RIADHA MLEMAVU WA AFRIKA KUSINI ALIYE MUUA MPENZI WAKE

HUYU NDO MWANAMKE ALIYE UWAWA HAPA ENZI ZA UHAI WAKE
 
Pistorius alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavukushiriki michezo ya olympic



Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amekamatwa na polisi na amekuwa akihojiwa kuhusu mauaji ya mpenzi wake nyumbani kwake mjini Pretoria.
Kulingana na vyombo vya habari, mkuu wa polisi, Sarah Mcira, aliambia wanahabari kuwa mwanamke aliyefariki nyumbani kwa mwanariadha huyo alipigwa risasi kwenye mkono wake na kichwani.
Hata hivyo hali iliyosababisha mauaji hayo bado haijulikani.
Duru zinasema kuwa Pistorius huenda alimuua Reeva Steenkamp kimakosa kwa kudhania kuwa ni mwizi aliyekuwa amemvamia.
Polisi wanasema wamemkamata mtu mwenye umri wa miaka 26, lakini hakuna thibitisho lolote kuwa ni Pistorius.Mshukiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani baadaye leo.
Pia ilithibitishwa kuwa mwanamke mmoja aliuawa nyumbani kwa Pistorius na kwamba alikuwa rafiki yake. Polisi walisema kuwa awali kulikuwa na visa kadhaa vilivyoriptiwa kutokea katika sehemu anakoishi Pistorius na kutajwa kuwa madai ya unyanyasaji au dhulma za kinyumbani.
Pistorius anasifika kama mwanaridha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki. Habari za mauaji ya mpenzi wake Pistorius zimewashangaza wengi Afrika Kusini kwani anasifika kama mwanaridha anayeiletea nchi hiyo sifa.
Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye visa vingi vya uhalifu duniani na watu wengi wanamiliki silaha za kujilinda.

Comments system

Disqus Shortname