LILE bifu la kugombania jina la Simba ambalo linawahusisha wasanii
nyota wa Bongo Fleva, Henry Samir ‘Mr Blue’ na Nasibu Abdul ‘Diamond’
limemuibua mkongwe Suleiman Msindi ‘Afande Sele’ ambaye alikuwa kwenye
mishe za siasa.
Afande Sele maarufu Mfalme wa Rymes, aliyekuwa akigombea Ubunge
katika Jimbo la Morogoro Mjini, amesema yeye ndiye mwanzilishi wa jina
hilo miaka mingi iliyopita.
“Hata ukimuuliza mtoto mdogo atakuambia, mimi ndiye Simba Dume. Mwaka
2008 nilifanya wimbo na P Funk Majani, unaitwa Simba Dume na nikaanza
kutumia hilo kutokea hapo, nawashauri waachane na mabifu yasiyo na
maana.
“Ni bora wote watatu tukutane, tufanye kolabo, kila mmoja aelezee
usimba wake kwenye mashairi, naamini itabamba na itakuwa na maana na
faida kwa kila mmoja na mashabiki wetu,” alidadavua Afande Sele.
Mtanzania
No comments:
Post a Comment