30 December 2015

WIZARA ZA MALIASILI NA UTALII, TAMISEMI NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA KUANZISHA PROGRAMU YA UPANDAJI MITI


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akizungumza kwenye kikao cha pamoja kati yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Januari Makamba (kulia) leo tarehe 29 Desemba 2015 katika ukumbi wa Selous Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuipa majukumu Kamati Maalum ya Wataalam ya kutengeneza andiko maalum litakalotumika kuandaa Programu ya pamoja ya kitaifa ya upandaji miti nchi nzima kuanzia mijini hadi vijijini kwa lengo la kuhifadhi na kuendeleza mazingira ikiwemo misitu. Kwa mujibu wa Prof. Maghembe Kamati hiyo imepewa wiki mbili kukamilisha kazi. Mpango huo utashirikisha pia Wizara ya TAMISEMI.

SOMA ZAIDI 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname