RIPOTI
zimesambaa kwamba wanamuziki nyota wawili wa Nigeria, Davido na Tekno,
huenda wanachangia penzi la mrembo wa Kitanzania, Agnes Masogange.
Mwezi
Novemba mwaka huu mwimbaji Davido ambaye alivuma na album ya Omo Baba
Olowo (Mtoto wa Tajiri) alijirusha na wasichana kadhaa wakati wa
bethidei yake na mmoja wao alikuwa Masogane na baadaye zikaenea habari
kwamba alikuwa mjamzito akitegemewa kumzalia Davido mtoto wa pili,
lakini habari hizo baadaye zikakanushwa.
Kitu
cha ajabu ni kwamba Masogange alianza kuweka na kufuta ujumbe
mbalimbali kwenye mtandao ukionyesha alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na
Tekno kwa kula naye bata katika hoteli moja nchini Afrika Kusini.
Tekno
naye alianza kutuma ujumbe kama huo, jambo lililowafanya mashabiki wake
kuamini alikuwa na uhusiano na msichana huyo. Hata hivyo, mwimbaji huyo
ameufuta ujumbe wote huo katika ukurasa wake.
CHANZO;GPL
No comments:
Post a Comment