Wabunge wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa wameonywa kutofanya
jambo lolote litakaloashiria kuvuruga Bunge wakati Rais John Magufuli
atakapolihutubia leo jioni.
Akiongea jana mjini Dodoma, Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape
Nnauye alisema kuwa Wabunge hao wa Ukawa wanapaswa kufahamu kuwa kitendo
chochote watakachofanya kwa lengo la kuvuruga hotuba hiyo ni kinyume
cha sheria na taratibu za Bunge na kwamba hawatavumiliwa.
Nape
alionesha kuwashangaa wabunge hao kudai kuwa hawamtambui Rais Magufuli
ili hali wanashiriki katika shughuli zote za Bunge ikiwa ni pamoja na
kumpigia kura Waziri Mkuu ambaye ameteuliwa na Rais huyohuyo wanaedai
hawamtambui.
Naye Mbunge wa jimbo la Nzega, Dkt Khamis Kigwangala
alisema kuwa wabunge wa Ukawa wana haki ya kuingia Bungeni na kukaa kwa
utulivu au kutoka nje endapo hawatakuwa tayari kusikiliza hotuba hiyo
lakini sio kuvuruga hali ya amani ili watanzania wasipate nafasi ya
kumsikiliza Rais.
“Hawawezi kuwanyima haki watanzania kumsikiliza
Rais wetu akiwa anatoa dira ya uelekeo wa Taifa letu,” alisema Khamis
Kingwangala.
Wabunge wa Ukawa jana walifanya mkutano na vyombo vya
habari na kueleza kuwa hawatakubali kumuona Rais wa Zanzibar, Dkt Ali
Mohamed Shein akiingia katika Bunge hilo leo kwa kuwa kipindi chake cha
urais Zanzibar kimekwisha. Walisisisitiza kuwa watafanya ‘jambo’ ambalo
hata hivyo hawakulitaja. Wabunge hao pia walisema kuwa
wamemuandikiabarua Spika wa Bunge kuhoji uhalali wa hotuba ya Rais
wakati Zanzibar bado haijampata Rais mpya.
No comments:
Post a Comment