15 November 2015

HAKIKA SASA SPIKA ANATOKA KATI YA HAWA WATATU....UNADHANI NANI ANAFAA KATI YA HAWA

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake Dkt Jakaya Mrisho Kikwete imepitia, imejadili na kupitisha majina ya wana-CCM watatu kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kamati Kuu imewateua;

1. Mhe Job Ndugai
2. Mhe Abdullah Ali Mwinyi.
3. Dr Tulia Ackson Mwansasu.

Majina hayo matatu yatapigiwa kura kesho tarehe 16th Nov 2015 katika kikao cha wabunge wa CCM ili lipatikane jina moja ambalo litapelekwa na Chama kwenye uchaguzi wa Uspika Bungeni.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname