Ni lazima wanachama wa vyama husika, yaani Chadema na CUF wahoji sababu za viongozi wao kujiweka kando kwa sababu walianza wote safari ya mapambano ya kile wanachokiita ‘kusaka mabadiliko’, lakini ghafla viongozi waliowaamini walishukia njiani.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk Willibrod Slaa alipoamua kuachana na chama hicho yaliibuka
maswali mengi kuliko majibu na hata Profesa Ibrahim Lipumba alipoukataa
wadhifa wake wa uenyekiti Taifa wa CUF kwa sababu tu Edward Lowassa
amepitishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kugombea urais, pia
watu walihoji.
Ni lazima wanachama wa vyama husika, yaani Chadema na CUF wahoji sababu za viongozi wao kujiweka kando kwa sababu walianza wote safari ya mapambano ya kile wanachokiita ‘kusaka mabadiliko’, lakini ghafla viongozi waliowaamini walishukia njiani.
Bora Dk Slaa na Profesa Lipumba walishukia njiani kwa sababu inayofanana ambayo ni ujio wa Lowassa na si kwa sababu mbaya yoyote inayovihusu vyama hivyo iliyofanyika miaka mingi iliyopita.
Kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru, yeye ameachana na chama hicho kwa madai kuwa hakina tena pumzi ya kuendelea kuongoza nchi.
Kingunge aliyedumu na Tanu na hatimaye CCM kwa miaka 61 alisema hatajiunga na chama chochote cha siasa, lakini hapo hapo akabainisha kuwa nusu karne ya utawala wa kuanzia uongozi wa chama tawala unatosha kwa kuwa madaraka yamewalewesha viongozi wa chama hicho.
Katika hoja zake alieleza kuwa Watanzania wengi wa kada mbalimbali kama wafanyakazi, wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo, wanafunzi, wasomi, wanawake na vijana wanataka mabadiliko na CCM haiwezi tena kuyaleta.
Alisema nchi imefika mahali pagumu kiuchumi kiasi kwamba wananchi sasa wanataka mabadiliko ambayo yanaweza kuletwa na chama kingine na watu wapya na siyo tena CCM.
Mzee huyu ambaye ni mshirika wa karibu wa Lowassa, pia aliupinga mchakato wa kupata mgombea urais wa CCM kule Dodoma kwamba uliwadhalilisha watia nia 38 waliorejesha fomu za uteuzi, jambo ambalo ni kinyume cha kanuni na taratibu za chama hicho.
Hoja zake nimezielewa, lakini nina maswali ambayo nimejiuliza baada ya kumsikiliza siku akitangaza kuachana na CCM.
Kama Kingunge anajua kuwa CCM imepoteza mwelekeo tena siyo jana wala juzi ni siku nyingi kwa mujibu wake, ni kwanini hakukihama chama hicho wakati huo.
Natambua kuwa CCM kimegusa kwa namna moja au nyingine maisha ya Watanzania wote katika nyakati mbalimbali. Kuna walioguswa nacho katika hali chanya na wengine hali hasi. Tangu nianze kuwa na akili timamu ya kufuatilia masuala mbalimbali ya nchi na vyama vya siasa sikuwahi kumsikia kama si kumwona Kingunge akitoa kauli za kukemea yanayofanywa na kilichokuwa chama chake, CCM.
Jaji Joseph Warioba ni kada wa CCM, lakini walau amekuwa akikikosoa chama hicho sanjari na Joseph Butiku na marehemu Peter Kisumo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye nao walau tumewaona wakizunguka mikoani kukemea ‘utumbo’ unaofanywa na baadhi ya viongozi ambao ni makada wa CCM.
Hawa wote tumewaona wakieleza ukweli na hata kama ni kwa unafiki, lakini wamesema, sasa Kingunge ulikuwa wapi mpaka kuibua leo tena nyuma ya pazia la ‘kukerwa na mchakato wa CCM kupata mgombea urais’.
Nchi imekwama, uchumi unaporomoka, wananchi wanalia shida na njaa, ajira hakuna na mambo mengine mengi, lakini Kingunge alikuwa kimya akisubiri 2015 ndipo aeleze hilo? Hapo ametundanganya mzee wetu huyu.
Kingunge anasema CCM ilikiuka katiba yake, sasa mbona chaguzi nyingi zilizopita chama hicho kimekiuka mengi ya kikatiba, mbona hakuwahi kusema?
Katika uchaguzi wa 1995 na 2005, rafu nyingi zilidaiwa kuchezwa katika mchakato wa CCM kupata mgombea wake wa urais mbona Kingunge alikuwa kimya?
Hivi kuchaguana kwa makundi ndani ya CCM kumeanza leo na hata hili suala la viongozi kupatikana kwa rushwa ni geni ndani ya chama hiki tawala?
Rushwa na makundi ndani ya CCM ni kama saratani inayokitafuna chama hicho taratibu na kwa muda mrefu vigogo wa chama hicho wamekuwa wakilipigia kelele, mbona Kingunge hatukumwona?
Ukweli ni kwamba Kingunge ni sehemu ya uozo unaofanyika CCM kwa sababu naye alikuwa ndani ya chama hicho kwa muda mrefu na wakati hayo yanatokea alikuwapo, hawezi kulikimbia hilo.
Hivi kama Lowassa angekuwa mgombea urais wa CCM, Kingunge angeachana na chama hicho?
Binafsi jibu ni hapana. Angeendelea kubaki ndani ya chama hicho na kauli zake alizozitoa ambazo nimeziandika hapo juu tusingezisikia tena, ghafla CCM ingekuwa safi!
Ndiyo maana siku chache baada ya Lowassa kutoswa, Kingunge aliibuka na kuuponda mchakato mzima wa CCM kupata mgombea urais, kueleza kuwa chama hicho kinamhitaji Lowassa kupata ushindi.
Iweje ahame chama kwa sababu ya mtu? Hilo ni tatizo jingine ninaloliona kwa Mzee Kingunge. Hivi akiwa CCM hata kama hakusema wazi alichukua jukumu gani kumweleza Rais Jakaya Kikwete juu ya kuporomoka kwa uchumi na maisha ya Watanzania?
Aaah! Hawa ndiyo wazee wetu bwana wakati mwingine wanaeleza ‘uozo’ waliougeuza asali wanapoona mambo yao au ya watu wao wa karibu hayaendi sawa.
0754 597315

No comments:
Post a Comment