Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Pemba jioni ya
leo kwenye kutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Gombani ya
Kale mjini Pemba.
Katika mkutano huo wa Kampeni,Dkt
Magufuli ameahidi kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano,atadumisha na
kuulinda Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ulioanzishwa na Waasisi wetu
akiwemo Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere pamoja na Abeid Amani
Karume.Dkt Magufuli kesho atahutubia kwenye mkutano mkubwa wa kampeni mjini
Unguja.
Wananchi wa Kisiwani Pemba wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa
Gombani ya Kale ,wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni wakimsikiliza
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kura kwa
wananchi hao.SOMA ZAIDI
No comments:
Post a Comment