Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrati (DP), Abdul Juma Mluya ameibuka na
kusema mazingira ya kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho,
Mchungaji Christopher Mtikila yamejaa utata huku akiweka wazi kwamba,
inavyoonekana aliuawa kabla ya ajali yenyewe.
Mtikila alifariki dunia
katika ajali ya gari aina ya Toyota Corolla namba T189 ARG, Oktoba 4,
2015 iliyotokea kwenye Kijiji cha Msolwa, Bagamoyo, Pwani. Wengine
watatu walijeruhiwa.
No comments:
Post a Comment