MTOTO wa staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford aitwaye Terry, analelewa
na mama yake mzazi wakati yeye akiwa bize na kampeni kuelekea uchaguzi
mkuu.
Shamsa akithibitisha jambo hilo, aliliambia gazeti hili kuwa amelazimika kumuacha mwanaye kwa bibi yake ili aende na kasi ya kampeni, lakini hujitahidi kuzungumza naye kwa simu kila siku ili kumfanya ajisikie vizuri.
“Namkumbuka sana mwanangu, lakini sina wasiwasi maana yupo kwenye mikono salama, tukipumzika kwa wiki mara moja au ndani ya wiki mbili huwa narudi Dar kumuona, unajua ndiyo harakati za kisiasa lazima nimwache kwa muda,” alisema Shamsa ambaye ni mwanachama wa Chadema.

No comments:
Post a Comment