Miili ya makumi waliopoteza maisha wakati wa mashambulizi hayo.
Hali ilivyokuwa eneo la tukiuo.
Ankara, Uturuki
Milipuko miwili imetokea wakati wa
mkutano wa hadhara wenye lengo la maandamano ya amani katikati mwa Mji
Mkuu wa Uturuki, Ankara asubuhi ya leo na kusababisha vifo vya watu
zaidi ya 52 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa vibaya.
Picha za televisheni zilionyesha watu waliokuwa na hofu na wengine
wakiwa wamelala chini wakiwa wametapakaa damu miilini mwao. Wakati duru
ya pili ya uchaguzi wa ubunge ikitarajiwa kufanyika mwezi ujao,
maandanmano hayo yalipangwa na vyama vya wafanyakazi wakitaka kumalizika
kwa mashambulizi yanayoendeshwa na serikali dhidi ya wanamgambo wa
Kikurdi.
No comments:
Post a Comment