21 September 2015

Mama janeth magufuli akonga nyoyo za watanzania ndani na nje ya nchi


 Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua mumewe Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kwenye  uchaguzi mkuu unaotarajiwa wa Oktoba 25 mwaka huu. 
Mara bada ya kuhutubia chumba chetu cha habari kilihemewa na simu za wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kuelezea furaha yao sio tu kwa kumuona jukwaani bali pia kwa kuongea kwa kujiamini. Mama Magufuli amekuwa haonekani sana kwa sababu ya kuuguza mgonjwa nyumbani kwao Chato. Wamesema wametiwa moyo sana na haiba ya Mama Magufuli na wameshangazwa kwa uwezo wake mkubwa wa kuongea mbele za watu bila woga na bila kumung'unya maneno. 
Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu
 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname