Siku moja nisiyopenda kuikumbuka nilitwa ofisini kwa bosi wangu na kukabidhiwa barua ya kufukuzwa kazi
Hiyo
ilikua ni baada ya uchunguzi wa miezi kdhaa wa kosa nililokua
nimelifanya bahati mbaya. Miezi mitatu nyuma nilimuingizia pesa mteja
kimakosa kwenye akaunti yake kiasi cha million mia tatu na hamsini
ambazo alitakiwa kuwekewa Mteja mwingine halali kupata pesa hizo.
Kama
humu ndani Kuna banker ataelewa nachokisema, kwamba makosa kama haya
benki ni kawaida sana. Ukigundua kosa kama hili unawahi una reverse hiyo
entry una m-credit anaetakiwa shida ni kama uliemwekea kimakosa akawahi
kuzichukua ndipo yanakukuta yaliyonikuta mimi.
Baada ya kufukuzwa kazi mke wangu alibadilika kabisa
Nilishuhudia yafuatayo:-
(1) Alitamka mimi ni mjinga ndio maana nimefukuzwa kazi.
(2) Chake kikawa chake tu.
(3) Akawa anawaambia wazi watoto kuwa kitu fulani kimenunuliwa na yeye na sio mimi.
(4)
Muda wa kurudi home ukabadilika sasa anarudi usiku mwingi, nampa kipigo
cha nguvu anazira na kukimbilia kwao, kwenye usuluhishi anawaambia
wasuluhishi kwamba mimi namuonea wivu kwa kuwa ana kazi mimi sina.
(5)
Niliuza Gari zangu mbili ili nipate mtaji wa kufanya biashara hivyo
nikawa sina Gari nilijua maadam wife ana Gari tutatumia wote maana hata
yeye wakati hana Gari alikua akitumia magari yangu.
Kinyume na matarajio hakutaka kabisa niguse Gari lake mimi nikawa mtu wa miguu.Majirani wakawa wanashangaa mfumo wetu wa maisha.
(6)
Life yetu ya bedroom ikawa imekufa no intimacy no love making nothing.
Alianza kidogo kidogo leo mara aseme anaumwa, kesho kachoka, hadi mwezi
unaisha. Nikaamua isiwe tabu nikaacha kuulizia tena, nae akawa
amepotezea moja kwa moja.
Hata
wazazi wangu aliwa mistreat sana wakawa hawaji tena kwangu, mama yangu
akawa ananitumia vitu kwa njia basi kutoka nyumbani kama mchele,
maharage, unga na kadhalika ili na mm nionekane nachangia.Wakuu siku ya
kufa nyani miti yote huteleza. Kila nilichojaribu kukifanya ili
nijinasue kinakwama, nakuta mtaji wote unakata naanza moja.Ilikatika
miaka minne nikiwa kwenye hali hii maana nilipata matatizo 2010. Mwaka
Jana kuna Dada mmoja tulisoma wote primary school akaamua kunisaidia,
huyu dada tulikutana Posta accidentally tukapeana contact
mimi nilishamsahau ila yeye alinikumbuka.
Baadae
akaniunganisha na mumewe ambae ni HR manager kwenye shirika fulani,
nikamwelezea ukweli wote na akaniingiza kaziniWife sikumwambia kuwa
nimepata kazi akaanza kuona nakuja na mahitaji ndani, nikawa naondoka
zangu alfajiri narudi usiku mwingi. Nikaita mafundi wakabomoa ukuta wote
wa fensi uliokua umeoza waliiba sana cement wakati wa ujenzi ukajengwa
upya, vitu vyote vilivyochoka ndani nikabadilisha. Wife alishangaa sana
ila akashindwa kuniuliza maana hadi hapo tulikua hatuongeleshani zaidi
ya salam za asubuhi na jioni tu basi.
Wana
jf siwezi kuwaficha sehemu niliyopata naingiza hela Mara kumi ya ile
kazi yangu ya benki, hii sikutokana na mshahara bali njia mbali mbali
katikati ya mwezi kitengo chetu tupo wanne,hali ikiwa nzuri huwa
tunagawana hadi laki mbili kila siku, kama hali ni mbaya tunagawana laki
moja kwa siku hii ni mbali na ile tunayogawana mwisho wa mwezi kama
million 3 each person mshahara ni mdogo tu ni laki saba tu kwa
mwezi.Maana mshikaji alisema anaweza kuniingiza kazini ila kama
mfanyakazi wa kawaida kwa kuwa benki nilifukuzwa hakukua na reference
wala background check so nikaamua kufuta kwenye CV kuwa nilifanya bank.
Nimeanza
mchakato wa talaka kupitia mwanasheria mmoja rafiki yangu, mwezi
January mwaka huu amemwandikia barua ya kumtaarifu uamuzi huo na copy
Ustawi wa jamii pia, baadae tutafungua shauri la talaka.Kinyume na
matarajio yangu wife kwa kuwa alishaƱichoka na hakuna kinachoendelea
kati yetu nilijua angekubali tu. Cha ajabu hivi sasa kupitia wazee wake
wameniita kikao zaidi ya Mara 6 sasa ili tusuluhishe tofauti zetuKawa
mpole sana, alidhan nitaendelea kuteseka milele
Wakuu
sasa sipo nyumbani kwa hasira ya mambo aliyonitendea hivi sasa sipo
nyumbani nimepanga upande wa nyumba nimeanza ujenzi ili nihamie. Kila
siku lazima nipite kwa watoto niwaone ndo niondoke. Nimesimama njia
panda, mm binafsi nilishaamua simtaki tena huyu mwanamke ila wazee na
viongozi wa dini tunakoabudu wanasema turudiane juzi mke wangu
alinipigia magoti tukiwa kikaoni kwamba nimsamehe, nifute kusudio la
kuomba talaka mahakamani. Wazazi wangu hawataki kusikia kabisa neno
msamahakwa matendo aliyotufanyia.
NB: Nimetaja kipato ili kuwapa mwanga na uelewa wa tatizo isichukuliwe vinginevyo
Nimesikia amepata matatizo kazini ila sina uhakika na taarifa hizo
No comments:
Post a Comment