Hii
sio mara ya kwanza kusikia kajitokeza binti flani na kudai kazaa au ana
ujauzito na staa flani wa muziki, movie, siasa au kingine chochote.
Sasa yule staa wa Nigeria ambae ndio yuko kwenye headlines na Diamond
Platnums kutokana na kolabo yao ya ‘number 1 rmx’ yaani Davido,
kimemkuta hiki cha huyu binti.
Mrembo huyu anaeishi Uingereza anaitwa Shanielle Sunshhine na
amenukuliwa akisema wazi anao ujauzito wa Davido, ni ujauzito wa mapacha
ulio na umri wa karibia miezi sita ambao ulitokana na kukutana kwao
mwaka 2013 wakati Davido alipofanya Tour Uingereza.
Pamoja na kwamba Davido amekua kimya wakati wote kuhusu hii ishu,
Shanielle amesema anakaribia kutoa vithibitisho vyote kwamba huo
ujauzito ni wa Davido.
No comments:
Post a Comment