Stephano akiwa na mpenzi wake mpenzi wake, Happy Merere baada ya kumvisha pete ya uchumba.KWELI! Baada ya mitandao mbalimbali kuripoti habari
zinazokinzana juu ya tukio la bwana harusi mtarajiwa aliyetajwa kwa jina
la Stephano kunaswa kwenye tukio la ujambazi muda mfupi baada ya
kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake, Happy Merere, bi. Harusi huyo
mtarajiwa ameibuka na kuanika ukweli wa mambo, Risasi Jumamosi lina full
stori.Stephano na wenzake watatu
walikamatwa Aprili 21, mwaka huu maeneo ya Red Cross jijini Dar akidaiwa
kuhusika katika tukio la kumpora fedha Mzungu mmoja raia wa kigeni pale
Kinondoni, Dar.
Kwenye tukio hilo, watuhumiwa hao, akiwemo Stephano au mume mtarajiwa wa Happy waliwekwa chini ya ulinzi na jeshi la polisi.
No comments:
Post a Comment