Wadau wa Forbes wamekuja
na ripoti yao nyingine ya utaftii ndani ya 2015, kama haujafahamu ni
kwamba idadi ya matajiri wenye asili ya Afrika ni 11 kati ya mabilionea
wote 1,826 duniani.
Jina la Aliko Dangote sio geni
kulisikia, ni tajiri ambaye yuko kwenye namba moja AFRIKA, anatokea
Nigeria, ni mfanyabiashara na muwekezaji mkubwa katika miradi kama ya
Cement, Sukari na miradi mingine, huyu unaambiwa ndio tajiri namba moja
mwenye asili ya Afrika duniani.
List ya mabilionea wote kumi hii hapa;
No.1:
Aliko Dangote, raia wa Nigeria ambaye ni mfanyabiashara wa mafuta,
cement ambapo moja ya miradi yake mikubwa unajengwa Tanzania.
No.2: Mohammed Al-Amoudi. Huyu ni raia wa Ethiopia, mfanyabiashara mkubwa wa mafuta.
No.3: Mike
Adenuga, raia wa Nigeria ambaye biashara yake kubwa ni mafuta na huduma
za Mawasiliano, anamiliki mtandao wa simu wa Globacom, huu ni wa pili
kwa ukubwa Nigeria.
No.4:
Isabel Dos Santos, raia wa Angola ambaye ni mtoto wa Rais wa zamani wa
nchi hiyo, Jose Eduardo dos Santos. Naye ni mwekezaji wa miradi
mbalimbali ikiwemo Kampuni za Mawasiliano na Mabenki pia.
No.5:
Oprah Winfrey, ni Mmarekani ambaye sehemu kubwa ya kipato chake
inatokana na TV show yake ambayo ni moja ya shows maarufu duniani.
No.6: Patrice Motsepe, raia wa South Africa. Ni mmoja wa wawekezaji wakubwa Afrika Kusini kwenye biashara ya madini.
No.7:
Folorunsho Alakija. Raia wa Nigeria ambaye aliacha kazi ya usekretari
na kujifunza masomo ya masuala ya fashion Uingereza, kwa sasa ni fashion
na kuwekeza kwenye miradi ya mafuta kumemfanya kuingia kwenye list hii.
No.8:
Theophilus Danjuma. Huyu ni mtu wa nne kwenye list hii kutoka Nigeria,
aliwahi kuwa Waziri wa Ulinzi Nigeria, kwa sasa utajiri wake unatokana
na biashara zake kuwekeza kwenye mafuta, pamoja na makampuni ya
usafirishaji wa majini.
No.9:
Mo Ibrahim. Anaishi Uingereza, ni mmoja ya wawekezaji kwenye makampuni
ya mawasiliano pia, alikuwa mmiliki wa Kampuni ya Celtel.
No.10: Tony Elumelu. Raia wa Nigeria, mtaalamu wa masuala ya uchumi na mfanyabiashara.
No comments:
Post a Comment