Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda Ernest Mangu, ameliambia gazeti
la The Citizen kuwa jina la Mohammed Emwazi maarufu kama Jihadi John
halikuwepo kwenye database ya watuhumiwa wa kigeni waliokamatwa na
kuondolewa nchini mwaka 2009. Kanusho hilo limeripotowa pia na BBC News.
Hata hivyo, Kamanda Mangu alisema kuwa hawezi kusema kwa uhakika kama
Jihadi John alishikiliwa na maafisa wa usalama nchini kwa sababu
watuhumiwa wa aina yake ni mabingwa wa kudanganya na wanaficha identity
zao na hufoji pasi za kusafiria. Gazeti hilo lilijaribu kumtafuta Waziri
wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai, DCP Diwani Athumani, lakini hawakupatikana.
Vyombo vya habari vya kimataifa vimeripoti kuwa Jihadi John alitaka
kuingia Tanzania mwaka 2009 kwa kutumia jina la Muhammad ibn Muazzam.
Alikuwa anasafiri na Mwingereza mwingine kwa jina Abu Talib na Mjerumani
aliyeitwa Omar. Hata hivyo, alizuiliwa kuingia nchini mara tuu baada ya
kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Taarifa zinadai kuwa maafisa wa usalama wa Tanzania walimkamata,
wakamhoji, wakamweka ndani na kesho yake wakampakia kwenye ndege na
kumrudisha kwao Uingereza kupitia Holland. Gazeti la The Independent la
Uingereza linadai kuwa Jihadi John alikamatwa nchini kwa amri ya MI5 ya
Uingereza
No comments:
Post a Comment