Balozi Mark Lippet akiwa na majeraha baada ya shambulizi.
Balozi
wa Marekani nchini Korea Kusini ameshambuliwa kwa kisu usoni na pia
katika kifundo cha mkono wake na mshambuliaji aliyekuwa akibwata
kuhusiana na suala la kugawanywa kwa kipande cha ardhi ya jumuiya yao.
Mara tu baada ya shambulio hilo Rais wa Marekani Barack Obama amemtakia uponaji wa haraka msaidizi
wake wa zamani Mark Lippert akimuombea uponaji wa haraka baada tu ya
shambulio lililofanywa wakati wa hotuba ya asubuhi.
Balozi
huyo mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa
upasuaji wa zaidi ya saa mbili ingawa madaktari wamethibitisha majeraha
yake hayatarishi maisha yake.
No comments:
Post a Comment