Wimbi la watu kumuunga mkono na kumshawishi Mbunge wa Monduli, Edward
Lowassa, kugombea nafasi ya urais wakati utakapofika, limezidi kupamba
moto na safari hii, ujumbe mzito kutoka Pemba unajiandaa kufanya hivyo.
Taarifa za maandalizi kwa wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kutoka Pemba kwenda Monduli kumshawishi Lowassa kugombea urais,
zimekuja siku chache baada ya baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM
Kanda ya Ziwa, kufanya hivyo wiki iliyopita.
Wananchi hao katika kutimiza dhamira yao, walimtuma Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya chama hicho taifa, Dk. Raphael Chegeni, kwenda
kumshawishi Lowassa ili awanie nafasi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Monduli jana, Mjumbe wa Halmashauri
ya chama hicho taifa, (NEC) kutoka Wilaya ya Chake Chake Pemba, Daud
Ismali, alisema amekwenda Monduli kumshawishi Lowassa kugombea nafasi ya
urais muda utakapofika.
Ismail ambaye ni mdogo wa Makamu wa Rais, marehemu, Dk. Omar Ally Juma,
alisema kwenda kwake Monduli ni kufanya maandalizi ya ujumbe mzito
utakao toka Pemba kwenda kumshawishi agombee urais.
“Watakuja kumwomba mheshimiwa Lowassa kugombea urais, uamuzi wa kugombea au kutogombea ni wake."
Akieleza kwanini waje kumshawishi Lowassa badala ya mtu mwingine, alisema ni kutokana na utendaji na uadilifu wake.
Pia alisema, “jina la mheshimiwa ni kubwa na siyo Pemba tu hata ukienda
Marekani ukiuliza ni jina gani linazungumzwa kuhusu urais utaambiwa ni
Lowassa.
“Ukienda mtaani kukusanya data za aina yoyote ile, jina linalotajwa kuwa linafaa kuwania nafasi hiyo ni la Lowassa,” alisema.
Pata bongo flava mbali mbali - http://rubega.com//index.php?a=explore
ReplyDelete