16 March 2015

HII HAPA TOP SEVEN YA MASTAA WA BONGO WANAOMILIKI MAGARI YA KIFAHARI

Asilimia Kubwa ya mastaa Wa bongo wamekuwa wakionekana wakijivinjari katika mitaa mbali mbali wakiwa katika magari ya kifahari. Lakini ukichunguza utagundua kuwa wengi Wa wasanii hao siyo wamiliki halali Wa magari hayo. Baadhi ya mastaa wanaosukuma ndinga za bei Kali apa bongo ni.

gari jipya la diamond platnumz
1: DIAMOND PLATNUM
Mwanamuziki anayedaiwa kuongoza kwa kuwa na gari la bei mbaya zaidi nchini ni Diamond Platnums ambaye kwa sasa anamiliki BMW X6 ambalo linauzwa kwa thamani ya dola 62,850 za marekani karibu shillingi million 150 za kibongo.

Gari la Lady Jaydee
2: LADY JAYDEE
Anayefuata ni mwanadada lady jaydee anayemiliki magari mawili ya kifahari ikiwemo Nissan Murrano alilonunua kwa thamani ya shilingi mil 60 miaka kadhaa iliyopita na Range rover E lenye thamani ya dola za kimarekani 60,000 sawa ni shilingi mil 100 .

Gari la AY
3: AY
Nafasi ya tatu imeshikwa na rapa mkongwe Ambwene yesaya anayemiliki Vogue sports lenye thamani ya sh92 miliion.

4: MASANJA MKANDAMIZAJI
Huyu anamiliki gari aina ya Land cruiser lenye thamani ya shillingi mil. 75

Gari la Mrisho Mpoto
5: MRISHO MPOTO
Namba tano inamilikiwa na mtaalamu Wa mashairi nchini, mrisho mpoto anayemiliki Toyota Prado new model yenye thamani ya shilling mil 65.

6: JACKLINE WOLPER
Kwa upande wake muigizaji jackline wolper anamiliki land cruiser Prado lenye thamani ya shillingi mil 65.

Gari la Wema sepetu
7: WEMA SEPETU
Nafasi ya saba inashikiliwa na mwigizaji wema sepetu anayemiliki BMW 545 yenye thamani ya shilingi million 56, pamoja Na Nissan murrano alilopewa Na aliyekuwa mchumba wake diamond lenye thamani ya shillingi mil 36.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname