Sharif
na wenzake; Shaibu Saidi maarufu kama “Mredii” (38), mkazi wa
Songambele, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara na Mussa Mangu (30),
Shangarai kwa Mrefu ( Arusha), Jalila Said (28), mkazi wa Babati, Sadiki
Jabir a.k.a “Msudani” (32), wa Dar es Salaam na Lang’ata, wilayani
Hai,
Karim Kihundwa (33), wa Kijiji cha Lawate, Wilaya ya Siha na Alli Musa
maarufu “Mjeshi”, wa Babati, mkoani Manyara, wanakabiliwa na kesi hiyo
ya mauaji namba 12 ya mwaka 2014.
Wakili
Mkuu Mfawidhi wa Jamhuri anayeongoza upande wa mashtaka, Neema Mwenda,
akisaidiwa na Abdallah Chavula, aliieleza mahakama hiyo mbele ya Jaji
Amaisario Munisi namna ambavyo washitakiwa hao walivyokutana na kudaiwa
kula njama za kutekeleza mauaji kwa kutumia mbinu shawishi za kumvutia
Msuya kukutana nao ili wamuuzie vipande vitatu vya madini ya Tanzanite.
“Mheshimiwa
Jaji, shauri hili namba 12 la mwaka 2014; la mauaji ya kukusudia, ni
kinyume cha kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16
iliyofanyiwa mapitio mwaka 2012; ambalo linakuja kwako kwa usikilizaji
wa awali…mbele yako ni washitakiwa saba wanaokabiliwa na mauaji ya
Erasto Msuya, ambao hata hivyo, nitaeleza mahakama yako namna
walivyotekeleza mpango huo,” alisema Wakili Chavula.
Baada
ya kuwasomea washtakiwa kosa la mauaji ya kukusudia linalowakabili,
Wakili Chavula alieleza mpango wa mauaji hayo unavyodaiwa kusukwa tangu
Julai 26, mwaka 2013.
Alidai
mshitakiwa wa kwanza, Sharif Athuman alikutana na mshitakiwa wa pili,
Shaibu maarufu “Mredii" Mererani na kumuomba amsaidie kutekeleza nia
yake ya kumuua Msuya.
“Baada
ya kukutana huko Mererani, Wilaya ya Simanjiro na kupanga mauaji hayo,
Julai 27, mwaka 2013, mshitakiwa wa pili (Shaibu), wa nne
(Jalila)
na wa saba (Mjeshi), walielekea Arusha mjini kukutana na mshitakiwa wa
kwanza, ambaye ni mpangaji wa mauaji hayo na wakakubaliana kumtafuta
mshitakiwa wa tano (Kihundwa) na mshitakiwa wa sita (Sadick) na baadaye
walikubaliana kununua pikipiki mbili kwa ajili ya kazi hiyo,” alidai.
Vilevile
alielezea namna mshitakiwa wa kwanza alivyodaiwa kufanikisha kusajiliwa
kwa namba za simu zilizotumika katika mauaji hayo akizitaja kuwa ni 0682 405323, 0788 275697, 0762 436644, 0768 201041 na 0788 642417 kwa jina la Motii Mongululu Mollel.
Aliendelea
kudai kuwa katika mpango huo, mshtakiwa wa kwanza, alimtumia pia mtu
aliyejiita, Adam Leale Mwangululu kununua pikipiki mbili aina ya Toyo,
yenye namba za usajili T 316 CLV ya rangi nyekundu kwa Sh. milioni 1.7
na nyingine ya King Lion, namba T 751 CKG kwa Sh. 1, 650,000 katika duka
moja, jijini Arusha.
“Alipokamilisha vitu hivyo, aliwaachia kazi washtakiwa... Agosti 6, mwaka 2013, mshtakiwa wa saba, akitumia simu namba 0682 405323 alimtumia ujumbe mfupi wa maandishi (sms), Msuya kwenye simu yake namba 0763 700000,
akijitambulisha kwamba yeye ni Motii Mongululu Mollel na kumweleza
anayo madini ya Tanzanite na anataka kufanya naye biashara; kwa hiyo
anaomba waonane. Siku hiyo hiyo, alimfuata Msuya na kumuuzia kipande
kimoja cha Tanzanite," alidai "Huyu mshitakiwa wa saba (Mjeshi)
alipouza kipande kimoja, alimweleza Msuya kwamba, anavyo vipande vingine
viwili vya Tanzanite na hawezi kumuuzia kwa siku hiyo, kwa sababu ni
vya watu wawili na mwenzake hayupo. Baadaye akampigia tena simu
akimwomba wakutane kesho yake eneo la Kia (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Kilimanjaro). Ilikuwa Agosti 7, mwaka 2013; Msuya alifika na gari
lake aina ya Range Rover lenye namba T 800 CKF na akawakuta Mjeshi na
Kihundwa,” alidai Wakili Chavula.
Aliongeza
kudai kuwa muda mfupi baada ya Msuya kuteremka kwenye gari lake na
kusalimiana na mshitakiwa wa saba, mshitakiwa wa tano, alitoa bunduki
aina ya SMG yenye namba KJ 10520 aliyokuwa ameificha kwenye koti lake na
kumpiga risasi na kufariki dunia.
Upande
wa mashtaka uliendelea kudai baada ya kumuua Msuya, polisi walifika
eneo la Mijohoroni, Wilaya ya Hai, karibu na Kia na kuukuta mwili wa
marehemu ukiwa chini, huku wauaji wakiwa wametelekeza maganda 22 ya
risasi.
Alidai Msuya aliuawa majira ya saa 6:30 mchana, eneo la Mijohoroni, kando kando ya Barabara Kuu ya Arusha-Moshi, karibu na Kia.
Alidai
polisi pia walikuta eneo la tukio, bastola yenye namba GLS 417T2 CAR
83271, mali ya Msuya na vitu vingine, ambavyo ni simu ya Samsung S5,
Ifone na koti la mshitakiwa wa tano (Kihundwa) likiwa limetelekezwa mita
chache kutoka eneo la tukio.
Pia
uliionyesha mahakama hiyo vielelezo vinavyodaiwa kuwa vilitumika
kutekeleza mauaji hayo, yakiwamo maganda 22 ya risasi za SMG, bastola, I
phone, jaketi (koti), kofia ngumu ya pikipiki, ramani yenye mchoro wa
eneo la tukio, taarifa ya uchunguzi wa daktari kuhusu kifo hicho,
pikipiki mbili zilizotumika na taarifa ya uchunguzi ya mtaalamu wa
silaha aliyethibitisha maganda ya risasi hizo yalitoka katika bunduki
iliyowasilishwa mahakamani.
Aidha,
upande wa mashtaka, uliieleza mahakama hiyo kwamba unakusudia
kuwapeleka mahakamani mashahidi 50 wa Jamhuri na vielelezo vingine
muhimu 40.
Upande wa utetezi katika kesi hiyo, unaongozwa na jopo la mawakili, John Lukindo anayemtetea mshitakiwa wa 4, 6 na wa 7.
Wakili
Majura Magafu anamtetea mshitakiwa wa pili na wa tano, huku Wakili
Emmanuel Safari mshitakiwa wa tatu na Wakili Hudson Ndusyepo mshitakiwa
wa kwanza.
Jaji
anayesikiliza kesi hiyo, Amaisario Munisi, alisema mahakama imemaliza
usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo na tarehe ya kikao kijacho cha
mahakama itapangwa na Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi na wadau
wa pande zote watajulishwa.
No comments:
Post a Comment