Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopita nilipata barua pepe kutoka kwa
mmoja wa wasomaji wangu aliyejitambulisha kwa jina moja la Joanitha.
Aliniandikia ujumbe mrefu sana juu ya kile kinachomsumbua kwenye maisha
yake ya kimapenzi na akaniomba nimsaidie ili aweze kuwa na amani.Ujumbe
wake huo ndiyo ulionisukuma kuandika makala haya kuelekea kwenye ile
siku muhimu sana kwa wapendanao ya Valentine’s Day.
Aliandika hivi: “Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 25. Nimekaa kwa
muda mrefu bila kuwa na mpenzi. Si kwamba napenda lakini nina kila
sababu ya kusema, sina bahati ya kupendwa.
“Niliwahi kumpenda kaka mmoja ambaye alikuwa akiutesa moyo wangu kwa
muda mrefu. Nilishindwa kujizuia na siku moja nilipokutana naye
nilimueleza bayana kilichokuwa kikiusumbua moyo wangu.
“Huwezi kuamini aliniambia wazi kuwa mimi siyo taipu yake, niliumia sana
baada ya kugundua kuwa nilimpenda lakini hakuwa na mapenzi na mimi.
“Sikuishia hapo, nikatokea kumpenda kijana mwingine, naye alinipotezea.
Sielewi nina kasoro gani. Mwenyewe nikijiangalia najiona ni msichana
ninayestahili kuwa na mpenzi lakini simpati wa kunipa faraja. Naomba
unisaidie anko.”
Ujumbe huo uliniumiza sana. Nikajua wapo wasichana wengi huko mtaani
wanaohitaji wapenzi lakini hawawapati. Pia kuna wanaume wanaotokea
kuwazimikia wasichana f’lani lakini kila wakijaribu kueleza hisia zao
wanajikuta wanatolewa nje.
Kimsingi hali hiyo imekuwa ikiwatesa wengi lakini sasa swali la
kujiuliza, ni kwa nini inatokea hivi? Inakuwaje mimi natokea kumpenda
msichana f’lani lakini yeye hana taimu na mimi? Wanaojiuliza swali hilo
ni wengi na kupata jibu kwa haraka ni ngumu hasa kama huna elimu ya
kutosha kuhusu mapenzi.
Iko hivi, mapenzi yana kitu f’lani cha ajabu. Unaweza kushangaa inatokea
mtu f’lani anakupenda sana lakini wewe huna taimu naye ila yupo ambaye
na wewe unampenda lakini wala hakujali. Wataalam wa mapenzi wanaeleza
kuwa, ni wachache sana waliopata bahati ya kuwapata watu wanaowapenda na
ndiyo maana wengi wamebaki wakiumia kwa kutopendwa na watu waliotokea
kuwapenda.
Watu kama hawa ndiyo wale ambao unawasikia wanaolewa na watu ambao
hawawapendi, wanakubali tu kwa kuwa hawana jinsi. Matokeo yake sasa
akiwa ndani ya ndoa kisha yule ambaye anampenda akajitokeza, ni rahisi
sana kusaliti.
Hata hivyo, wale wasio na bahati ya kupendwa kama ilivyo kwa Joanitha
wanatakiwa kujua kwamba, mapenzi yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu.
Unaweza kukaa muda mrefu bila kuwa na mpenzi lakini huwezi kujua Mungu
ana sababu gani.
Huenda hao ambao wewe unawapenda lakini wao wanakupotezea, siyo wale
walipangiwa kuwa na wewe na endapo utalazimisha utakuja kujuta
baadaye.Hatukatazwi kueleza hisia zetu kwa wale tuwapendao lakini
tutarajie pia majibu hasi. Ujue kwamba huna haki ya kupendwa na kila
utakayetokea kumpenda hivyo ikitokea umekosa uliyempenda, huna sababu ya
kuumia.
Chukulia ni jambo la kawaida na huenda hiyo ndiyo safari ya kuelekea
kumpata mtu atakayekupenda kwa dhati.Tuepuke kulazimisha kupendwa.
Ukiona dalili kwamba unampenda lakini yeye hana chembe ya mapenzi kwako,
kuwa mpole na muache. Nasema hivi kwa kuwa, wapo ambao wakitokea
kupenda watafanya wawezavyo wafurahishe nafasi zao.
Hiyo ni hatari na nakuhakikishia kwamba, huwezi kupata penzi la kweli na
badala yake utakuwa ni mtu wa kutendwa kila siku. Utasalitiwa,
utaudhiwa na kamwe hutapata kile ulichokitarajia. Kwa nini? Kwa sababu
uliyelazimisha awe na wewe, hakupendi kabisa.
Happy Valentine’s Day.
Credit GPL
sexy girl n i like it
ReplyDeleteJudi Online
Judi Bola
Taruhan Bola Online
Agen Judi Bola