Miaka kadhaa iliyopita, Diamond Platnumz alikuwa kijana mwenye ndoto
kama underground wengine wa muziki walivyo na hasira ya kutoka.
Story hii ni kwa nguvu ya Bongo 5.
Kutoka kwenye familia ya kawaida (kama zilivyo familia nyingi za
Kitanzania), Diamond alikuwa akihaha huku na kule kutafuta fedha ya
kuingia studio.
Fast forward – kwa kuungaunga hivyo hivyo alifanikiwa kurekodi wimbo uliokuja kubadilisha maisha yake, ‘Kamwambie’.
Ni wimbo aliouandika kwa hisia kutokana na kuhusisha kisa cha kweli cha
kuachwa na msichana. Ni kipindi hiki ambacho ‘Kamwambie’ inafanya vizuri
ndipo mapito ya Diamond na Wema yaligongana.
“Mi na Diamond tuliwahi kukutana mara moja tu Bilicanaz na hatukuwahi
kusalimiana kabla ya kuanza uhusiano lakini tulikuwa tunaangalia sana,
so nakumbuka alikuwa yupo smoking room kwahiyo tukawa tumepeana migongo,
nilikuwa na rafiki zangu wawili,” Wema aliiambia Bongo5 mwaka juzi.
“Nikamuona akaniona yeye alikuwa na rafiki yake, hatujasaliamija
hatujafanya chochote mimi nimechukua vinywaji tukatoka nje na marafiki
zangu tumesimama hapo nje nikawa naambiwa ‘yule ndio ameimba Kamwambie’
kipindi hicho nilikuwa namuona wa ajabu sana ila tu alijiseksisha kiasi
fulani.”
Na kweli kwa kipindi hicho, pamoja na kuanza kuwa na jina kubwa, Diamond
alikuwa bado hajaupgrade swagga zake huku Wema Sepetu akiwa kwenye
kipindi ambacho kila mwanaume alikuwa na ndoto ya kuwa naye.
Kwa maana nyingine kipindi hicho Wema alimuona kama mtu asiye na hadhi ya kuwa naye.
Fast forward tena – baada ya kuachana na Chaz Baba, Diamond na
Wema wakawa wapenzi. Ikawa couple moja yenye nguvu sana japo ni Wema
ndiye aliyekuwa na nguvu zaidi kuliko mwenzie.
Pamoja na kuendelea kutoa hits mfululizo ikiwemo ‘Mbagala’ na zingine
zilizofuata, Diamond alitumia uhusiano wake na Wema kulibrand na kulipa
nguvu zaidi jina lake. Alifanikiwa kwa hilo.
Fast forward kwa mara nyingine – mwaka 2014 – Diamond akaja kuwa
msanii asiyehitaji tena kujitambulisha akiwa katika nchi yoyote Afrika
kutokana na mafanikio aliyoyapata.
Kisha couple hiyo iliyokuwa na nguvu zaidi Afrika Mashariki ikaja kuvunjika.
Diamond akaangukia kwenye penzi la mwanamke tajiri, mrembo na mpenda
skendo kama yeye mwenyewe, Zari aka The Bosslady wa Uganda. Wawili hao
wanadaiwa kutarajia kupata mtoto.
Uhusiano wao ukawa gumzo si tu Tanzania, bali Afrika Mashariki nzima.
Lakini upande mwingine wa Wema mambo ni tofauti kidogo. Kwa muda sasa,
Wema amekuwa hatengenezi tena headlines kama mwanzo ukilinganisha na
kipindi kile yupo na Diamond. Habari kubwa na ya pekee iliyoandikwa hivi
karibuni ni movie yake na muigizaji wa Ghana, Van Vicker.
Mbaya zaidi historia inaonesha kuwa Wema amefanikiwa kuwa na ushawishi
huo kutokana na kuwa mtu wa kuandikwa sana kwenye magazeti ya udaku.
Sioni tena ile nguvu yake kama mwanzo. Hilo linanifanya nijiulize kuwa
kuvunjika kwa uhusiano wao kumekuwa na madhara makubwa zaidi kwa Wema
kuliko kwa Diamond? Wema ndiye aliyekuwa akihitaji zaidi uhusiano na
Diamond ili ushawishi wake uendelee kuwa pale pale?
Nakubali kuwa Wema Sepetu ni brand inayojitegemea na kwa njia sahihi
bado ataendelea kufanikiwa kisanaa, lakini ukweli unaonekana kuwa
hazungumziwi sana kama zamani.
Wewe una mtazamo gani? Funguka hapo chini.
No comments:
Post a Comment