BAADA ya kukiri kwa mdomo wake kutumia madawa ya
kulevya ‘unga’ na baadaye ‘kustaafu’, madawa hayohayo yamemletea msanii
Rehema Chalamila ‘Ray C’ ‘msala’ ambao umemfanya yeye mwenyewe, kwa
hiyari yake ajisalimishe polisi.
Hivi karibuni, Ray C alijikuta akiangua kilio ndani ya Kituo cha
Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar baada ya kuhusishwa na ishu ya
uuzaji wa unga.
KAWE DARAJANI
Chanzo hicho kilinyetisha kwamba,
siku ya tukio, wakati Ray C akitokea nyumbani kwake, alipofika maeneo ya
Kawe Darajani aliona pikipiki ikimfukuzia na baadaye ikampita na
‘kumbloku’.
Ilisemekana kwamba baada ya kusimama, jamaa alishuka
kwenye pikipiki kisha akamwambia aegeshe pembeni gari lake aina ya
Toyota Carina TI.
Chanzo kilidai kwamba, Ray C alikataa kufanya hivyo kwa kuhisi aliyekuwa akimwamrisha ni jambazi.
“Ray C aliamua kuondoa gari kwa kulazimisha ambapo alimkwepa jamaa huyo
kisha kukanyaga mafuta ambapo gari liliondoka kwa kasi,” alisema.
LUGALO
Ilisemekana kwamba baada ya kufika kwenye
kituo cha daladala cha Lugalo, alisimama na jamaa huyo aliyekuwa
akimfukuzia akaegesha pikipiki mbele yake na kumtaka Ray C ashuke ndani
ya gari kwani alitaka kulipekua akimwambia kuwa alikuwa amebeba unga.
Ishu hiyo ilizidi kumtia Ray C wasiwasi na kumuuliza jamaa huyo ni nani ambapo alisema kuwa yeye ni askari.
Kwa kuwa hakuwa na sare, Ray C hakuamini jambo lililosababisha jamaa huyo kumuonesha kitambulisho kilichokuwa kimechakaa.
MAELEWANO YASHINDIKANA
Baada ya kuona hivyo, Ray
C alimwambia waongozane hadi Kituo cha Polisi cha Oysterbay lakini
jamaa huyo alikataa na kumtaka waende Kawe jambo ambalo Ray C alishindwa
kuafikiana nalo na kuondoa gari lake akimwambia waambatane hadi Kituo
Kidogo cha Polisi cha Mwenge.
Jamaa huyo alionekana kutotaka kwenda hivyo Ray C aliondoa gari kwa
kasi na kuelekea Mwenge ambako alikuwa akiomba msaada kwa matrafiki na
alipoona wanachelewa aliondoa gari kumkimbia jamaa huyo.
Ilisemekana
kwamba awali alitaka kukimbilia Kituo cha Polisi cha Mwenge lakini
alipoona kuna msongamano alikimbia kwenda kujisalimisha Mabatini huku
akiangua kilio.
BOFYA HAPA KUMSIKIA RAY C
Baada ya kushibishwa taarifa hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Ray C ambaye alielezea mkasa mzima.
Alifunguka: “Ni kweli ulivyoambiwa tulitoka Lugalo na kuelekea Mwenge
baada ya kufika kwenye makutano ya Mwenge niliwaona askari wawili na
trafiki akiwa pembeni, nikawasimamisha na kuwaeleza.
“Askari mmoja alikubali kupanda kwenye gari langu nikaenda naye hadi Mabatini.
“Baada ya kufika Mabatini nilieleza kila kitu kwa mkuu wa kituo hivyo akaniambia nisiwe na wasiwasi.
“Bada ya hapo mkuu wa kituo aliita askari wa kike na wa kiume
nikaongozana nao hadi katika gari langu na kupekua kila sehemu lakini
wakasema hapakuwa na chochote kibovu, hivyo nikawa nalia tu na mkuu wa
kituo akaniomba ninyamaze na kuniruhusu nikaondoka zangu kwenda
Hospitali ya Mwananyamala kumeza dawa.
No comments:
Post a Comment