![]() |
Baba
mtarajiwa amezungumza kwa mara ya kwanza juu ya kuishi bila kuwa na uso
na kwa namna gani anahofia juu ya hali atakayozaliwa mtoto wake
mtarajiwa.Anaitwa Mohammad Latif Khatana, 32, kutoka Kashmir, India,
hawezi kuona wala kufanya kazi kutokana na ngozi zilizofunika uso wake.
Watu humkimbia barabarani kutokana na hali yake huku wakionekana
kuogopeshwa nayo.
|
Kwa
sasa ni mwenye faraja kutokana na ukweli kwamba mke wake ni mjamzito wa
miezi saba, ila ana hofu labda huenda mtoto wake anaweza kuzailiwa
akiwa anfanana naye. Alisema: “Naingoja kwa hamu hii hali ya kuwa baba
na kupata furaha ya maisha. Ila nahofu kila siku na kusali ili mwanangu
asije kuzaliwa kama mimi.”
Latif, ambaye anaishi milimani na mke wake mwenye miaka 25 aitwaye
Salima, eneo la Tuli Bana, ndani ya Jammu and Kashmir, huwa anatembea
mpaka Srinagar mara nne kwa mwaka kwa ajili ya kuomba misaada na ili
kupata hela.
Anasema:
“Mama yangu bado analia kila aniangaliapo, anajiona kama mtu mwenye
kosa na anashindwa kuelewa kwa nini mtoto wake wa mwisho amekuwa hivi.”
Latif ni mdogo kati ya wakaka wawili na dada watatu huku yeye pekee akiwa na tatizo hilo.
Bila ndugu zake angeweza kuishi maisha ya upweke sana udogoni kutokana na kutokuwa na marafiki.
“Hakuna aliyetaka kucheza na mimi utotoni,” akaongeza. “Wavulana
kijijini kwangu walikuwa wananipiga na kunitesa kila siku. Nilipoteza
jicho langu la kushoto nilipokuwa na miaka minane na wakawa wananiita
mjinga mwenye jicho moja.”
Alipokuwa kijana Latif alikumbana na changamoto mbalimbali za
kimaisha. Ni mtu mwenye nguvu zake ila kutokana na kushindwa kuwa anaona
na kwa namna uso wake ulivyo hakuna aliyeweza kumpa kazi. Alisema:
“Ningependa kufanya kazi ya uhakika kama wanaume wengine wanavyofanya
ili kuweza kuzitunza familia zao, ingenifanya nijisikie fahari sana, ila
hakuna aliyenipa nafasi. Inabidi niombe na naamini watu wanaweza
nisaidia ili niweze kulisha familia yangu.”
Miaka
minne iliyopita Latif alikutana na mwanamke wa maisha yake, awali
wazazi wake walijitahidi sana kumtafutia mke ila hakuna msichana
liyejitokeza, mpaka Latif aliposikia kuhusu Salima.
“Mke
wangu ana mguu mmoja tu na kwa muda mrefu amekuwa akitafuta mume, punde
tulipokutana tulijua tulikuwa sahihi kwa kila mmoja wetu,” anakumbuka.
“Wote tulikuwa hatujakamilika, hakika tuliendana.”
Walioana kwenye harusi ya Kiislamu wakiwa na wageni 400 mnamo August 2008 na wamekuwa wenye furaha toka kipindi hicho.
Akaongeza: “Najiona nimebarikiwa sana kwa kukutana na Salima, ni mwanamke mzuri kwangu.
“Sasa
naona kawaida nina mke, ni kitu kikamilifu zaidi ya awali. Na sasa ana
ujauzito wa mtoto wetu wa kwanza nina furaha sana. Haijalishi kwa namna
yoyote ile nnavyoonekana ila sasa ni mwanaume mwenye furaha.”
Ila Latif, ambaye hana maumivu na hapati matibabu yoyote, anahofu
mtoto wake kama anaweza kuzaliwa na hali kama aliyonayo yeye.
Anasema: “Hatuna uwezo wa kumuona daktari, sisi ni masikini sana.
Hakuna daktari kwa siku za nyuma aliyenieleza nisipate mtoto. Ninakuwa
na tumaini na kuomba kwamba mtoto wetu atakuwa mwenye afya.”
Kaka yake na Latif aliamua kuuza sehemu ya ardhi miaka minane
iliyopita ili aweze kulipia safari ya kwenda kumuona daktari ila
hakukuwa na namna ambayo wangeweza kuifanya.
Anakumbuka: “Daktari aliniambia kwamba hali yangu ilitokana na
mionzi ya jua wakati mama alipokuwa na ujauzito wangu. Ila sijui kama
nahitaji kumuamini.
“Na sasa kuna vitu vingi vinanijia kichwani mwangu kwamba kufanya
upasuaji inaweza kuwa ni kitu cha hatari sana. Nimepoteza tumaini lote
la msaada. “Hivi ndivyo nitakavyokuwa daiama.”
HAKIKA KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA na pia tukumbuke BINADAMU HUJAFA HUJAUMBIKA
source-danchibo
No comments:
Post a Comment