PAMOJA
na kuonekana kama mchezaji mtukutu uwanjani, lakini Mario Baloteli
ameonyesha ni mtu anayejali masuala ya elimu baada ya kuposti ujumbe
mzuri wa kuwatakia kila la heri wanafunzi wakirejea shuleni wiki hii.
Mshambuliaji
huyo wa Liverpool ameandika kwenye akaunti yake ya Instagram ujumbe
usemao: "Hi watoto, leo mnaanza shule kwenye nchi nyingi. Ni kama mwanzo
wa msimu kwenye soka. Huo ni wakati wa kufanya vizuri ili kujenga
mustakabali mzuri wa maisha yako. Kila la heri!'
Ujumbe huo ameuambatanisha na video fupi, amnayo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliyewahi kuchezea pia Manchester City, Inter Milan na AC Milan amesema: "Soma kwa bidii na chez a kwa bidii, nawatakia watoto wote kila la heri katika siku yako ya kwanza shule,".
No comments:
Post a Comment