Msanii wa Bongo fleva aliyetamba na hits
Song kibao Q chillah amefunguka na kusema kuwa ameacha kweli kutumia
madawa ya kulevya na kamwe hawezi kurudia tena maana madawa hayo
yalimfanya kuwa na maisha ya ajabu,kama kuona kila mtu ni adui
yake,kutokuwa na amani Q Chillah amefunguka hayo leo alipokuwa akichat
Live katika ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni
Live kinachofanywa kila siku ya Jumatano kuanzia saa sita mchana.
Q Chillah amesema toka ameeacha kutumia
madawa hayo ya kulevya kwa sasa ni mwaka wa tatu hivyo anawashauri
vijana kutojaribu wala kushawishika kuingia katika matumizi ya dawa za
kulevya hivyo wanapaswa kujitambua na kutambua dhamani yao kama vijana
na kujua kuwa taifa linawategemea hivyo wakiingia katika matumizi ya
dawa za kulevya watashindwa kutimiza ndoto zao nyingi na kuharibikiwa
kimaisha.
Mbali na kuzungumzia juu ya matumiz ya
dawa za kulevya pia Q Chillah ameweka wazi mikakati yake ya kurudi tena
katika game la Bongo Fleva na kuweza kushika hatamu katika muziki huo
kutokana na uwezo wake katika muziki,hivyo amenza kwa kuachia wimbo wake
mpya alioufanya na msanii Mb dogy,wimbo huo ambao leo umetambulishwa
katika kipindi cha Power Jams ya East Africa Radio unakwenda kwa jina la
Nipende Nikupende.
Ni kweli nilikuwa kimya katika muziki
kutokana na matatizo ya hapa na pale hivyo sikuacha muziki bali
nilianguka kimuziki lakini leo ndio nimerudi rasmi katika game na
nimetambulisha wimbo mpya niliofanya na Mb Dogy hivyo mashabiki zangu
kaeni mkao wa kula sasa.
SIJAROGWA NA DIAMOND ILA NAMKUBALI
Q Chillah amefunguka na kusema kuwa
baadhi ya vyombo vya habari na waandishi walimkariri vibaya ila
hajarogwa na msanii yoyote yule na nyota ya msanii Diamond kwa sasa
imewaka kwake ndio maana anafanya vizuri maana mwenyezi mungu ndiye
kamfungulia njia ya yeye kuweza kuwika na kufanya vizuri kwa sasa na
hakuna uchawi kama amabvyo baadhi ya watu wanavyosema.
"Hapana sikweli Diamond hanirogi bali
Mungu kamfungulia njia na daima nitasapoti kazi za wenzangu,tukumbuke
kuwa mchawi Mungu binaadam njia tu namkubali Diamond kama ambavyo watu
wenginewanavyomkubali"
Baadhi ya waandishi wa habari
wamekurupuka na hizo habari ila mimi siamini saaana nyota,naamini katika
uwezo wa mtu sababu bila uwezo binafsi nyota haiwezi onekana hata
kidogo,hivyo hata Diamond ameonyesha uwezo wake binafsi ndio maana
ameweza kufungua njia na kufika mbele zaidi kimuziki ila siamini uchawi
namwamini mungu

No comments:
Post a Comment