Nyota
ya Wizkid imeendelea kung’aa baada ya kuoneka akijiachia sambamba na
mwanamuziki Chris Brown pamoja na mchumba wake mwanamitindo Karrueche
Tran ikiwa ni siku chache kupita tangu wawili hao waingie studio kufanya
kolabo.
Tukio hilo lililotokea ijumaa ya juni 20 nje
kidogo ya hoteli ya The SLS iliyopo eneo la Beverly Hills mjini
California huku habari hiyo ikipewa uzito na tovuti maarufu ya UK
Dailymail. ”Hey there : The rapper was seen greeting popular Nigerian artist Wizkid outside the hotel” uliandika mtandao huo.
Hii sio mara ya kwanza kwa Wizkid kuonekana akihang out na mastaa nyota wa marekani kama vile Akon,Big Sean, Justin Bieber, Tyga, Ty Dollar pamoja na staa wa filamu za Fast & Furious Tyrese Gibson.
No comments:
Post a Comment