Uganda:Mashoga,wasagaji kufungwa maisha Safi sanaaaaa!!!!!!!!!!
Uganda imepitisha mswada unaopinga mapenzi ya jinsia moja.
Iwapo Rais Yoweri Museveni ataidhinisha sheria hiyo inamaanisha atakayepatkana na hatia atahukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Mswaada
huo uliopitishwa na bunge siku ya Ijumaa halikadhalika inasema mtu
yeyote aliye na taarifa za watu wanoshiriki mapenzi ya jinsia moja na
kushindwa kuripoti habari hizo kwa maafisa wa polisi atafungwa gerezeni
maisha.
Wakati hu huo bunge hilo hilo la Uganda siku ya Alhamisi liliidhinisha mswaada unaopiga marufuku maonyesho ya picha za chafu.
Mswada huo unaharamisha kitu chochote
kitakachoonyesha sehemu nyeti kama vile matiti, mapaja, makalio au tabia
yoyote inayozua uchu wa mapenzi.
Kulingana na mswada huo, sheria
iliyopo sasa kuhusu picha chafu haihusu zaidi picha hizo bali linahusu
uchapishaji ,mawasiliano, taarifa , burudani, maonyesho katika kumbi za
kuigizia, miziki inyochezwa katika vyombo vya habari, densi, sanaa,
mitindo na picha za runinga.
Mapema mwaka huu Waziri wa maadili wa
Uganda, Simon Lokodo, alipendekeza kuwa mwanamke yeyote anayevalia nguo
ambayo inafika juu ya magoti anatakiwa kukamtwa na kuadhibiwa kisheria.
Mswada huo unahitaji kuidhinishwa na Rais kabla ya kufanywa sheria.
Uganda ni nchi inayoshikilia mawazo ya
kihafidhina yaani isiyopendelea mageuzi katika mawazo na inaandaa
sheria ya kuwaadhibu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ikijumuisha
hukumu ya kifo katika baadhi ya kesi.
No comments:
Post a Comment