Jeneza lenye mwili wa Clement Mabina likiwa mbele ya waombolezaji. |
Hata hivyo, mazishini hapo vyanzo vyetu vilisema kuwa marehemu Mabina alizuiwa na mkewe na kiongozi mmoja wa Kituo cha Polisi cha Kisesa akiambiwa asiende kwenye shamba lililotokea muaji yake lakini ilishindikana.
Waombolezaji wakiwa katika ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Mabina kwenye uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza.
Ilielezwa na chanzo chetu kuwa siku ta
tukio marehemu akiwa nyumbani aliambiwa na vijana wake aliowatuma kwenda
kuweka mipaka kwenye shamba hilo, kuwa wamezuiwa kupanda miti na
wakazi wa eneo.
Habari zinasema baada ya kupokea taarifa hiyo marehemu aliingia ndani
kisha akatoka ambapo mkewe alimzuia ikiwa ni pamoja na kuficha funguo
za gari lakini bila mafanikio.Ikazidi kuelezwa kuwa baada ya kukosa funguo, marehemu aliamua kupanda gari dogo la abiria na kuelekea eneo la tukio. Alipofika alikutana na kundi la wananchi wakiwa na silaha za jadi (mapanga na mikuki).
“Kabla ya kufika shambani gari hilo (Hiace) lilishambuliwa kwa mawe na watu hao, vijana waliokuwa na marehemu wakakimbia,” kilisema chanzo.
Habari zinasema baada ya kuona hivyo, Mabina akalazimika kukimbia na kwenda kujificha lakaini akaonekana na kushambuliwa.
Hata hivyo, habari za uhakika zinaeleza kuwa watuhumiwa waliomuua Mabina ni kundi la wachimbaji wa mawe na changarawe katika eneo hilo lililokuwa likimilikiwa na marehemu.
Mabina aliuawa na wananchi wanaodaiwa wenye hasira kwa kupigwa mawe na kukatwakatwa kwa mapanga kichwani Desemba 15, mwaka huu, saa 6:45 katika Kijiji cha Kanyama, Kata ya Kisesa Magu na kuzikwa juzi.
Miongoni mwa watu waliohudhuria mazishi ni pamoja na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, Waziri Nchi Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu, Steven Wasira, Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo, kaka wa Rais Kikwete, Seleman Kikwete, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli na makada wa CCM, Getrude Mongela na William Ngeleja.
-GPL
No comments:
Post a Comment