01 December 2013

SHOW YA MTIKISIKO YAFUNIKA MBAYA...HUKU MADEE AKIVAMIWA NA MLEVI JUKWAANI, SHILOLE AOKOLEWA NA POLISI ,SHOW YAVUNJA REKODI YA WATU HUKO IRINGA


Maelfu  ya  wakazi  wa mkoa wa Iringa wakiwa ndani ya show ya Mtikisiko 2013 Iringa
Wadau wa mtandao  huu wakiwa  katika show  ya mtikisiko 2013  na radio Ebony  Fm ndani ya uwanja wa Samora
Msanii  Madee a.k.a mzee wa nani kamwaga Pombe yangu akipagawisha katika  show ya Mtikisiko Iringa
 msanii Madee  a.k.a 'Pombe yangu akiwa amevamiwa na mlevi wa ukweli jukwaani
Kikosi  kazi  cha  ma DJ  wa ukweli  wakifanya mavituzz
Umati kama  huu haujapata  kutokea ndani ya uwanja  wa Samora
Mtangazaji wa  Radio  Ebony Fm Raymond Francis  kushoto akiikubali show  ya Mtikisiko na nyomi ya  watu katika  uwanja  wa samora
Msanii  Shilole  katikati akionyesha  show  na  wachezaji  wake
Polisi  akimthibiti msanii Shilole ambae  aliamua kuruka jukwaani na  kuwafuata  mashabiki  wake ambao walipandwa na mzuka na kucheza nae
hapa  polisi  wakimrudisha  jukwaani msanii Shilole ambae  alikuwa ni ngunzo katika  show  hiyo ya Mtikisiko
Njemba  zikimvizia msanii Shilole  ili kumgusa huku  polisi  wakiwa wameweka ulinzi  mkali
Mtangazaji wa Radio  Ebony Fm Bw Alen Philip kulia  akiwa na mdau  wa vipindi vyake  na show ya Mtikisiko
Msanii baba  Revo akipagawisha
Msanii baba  Revo akiwa amenogewa na mrembo wa Iringa
hapa akiwa amevua  nguo ya juu
Msanii Squza awakumbusha  wana  Iringa
Watangazaji wa radio Ebony Fm  Sogg na Aisha a. k.a Baba na Mwana wakiwa katika furaha  kubwa ya Mtikisiko
Mtangazaji wa Radio Nuru Fm Emmanuel Mwansasu akifuatilia show  ya Mtikisiko 2013

 ONYESHO kubwa la kufunga mwaka la Mtikisiko na radio Ebony Fm 2013 Iringa  limevunja  rekodi  ya umati  wa watu  kuingia katika  uwanja  wa Samora toka show kama  hizo zilipoanza katika uwanja  huo kwa zaidi ya miaka minne  sasa .


Mbali ya  Show   hiyo kupata  umati mkubwa wa watu pia  idadi  kubwa ya wasanii  walioletwa katika  show  hiyo  walijikuta  si lolote mbele ya msanii Madee  kupitia  wimbo wake wa Nani kamwaga  pombe  yangu baada ya  shabiki  wake ambae  alikuwa amelewa  chakali kumvamia msanii  huyo jukwaani wakati akiimba  wimbo  huo wa nani kamwaga pombe yangu huku mlevi   huyo akiitikia ni mimi nimemwaga  pombe  yako na nipo tayari  kukumwagia na hii.

Mlevi  huyo ambae  alikuwa na chupa ya pombe mkononi alianza kumkumbatia msanii  huyo huku akiangua  kilio kiasi cha askari  na  timu ya ulinzi  uwanjani hapo kupanda  jukwaani na kumng'amua  katika mwili wa msanii Madee

Wakati msanii Madee akivamiwa jukwaani na mlevi bado   watu  wa ulinzi  walijikuta katika wakati mgumu kumthibiti msanii  huyo ambae alionyesha  kupendwa zaidi na mashabiki uwanjani hapo.

Kama  haitoshi  msanii Shilole  pia  aliwapa  wakati mgumu  polisi  baada ya  kuruka  jukwaani na kuwafuata mashabiki   hali iliyozua hofu  zaidi uwanjani hapo kutokana na kundi la vijana waliopangwa na mzuka wa  nyimbo za msanii  huyo  kutaka kumng'ang'ania  kiuno kwa kila mmoja akitaka  kushika mwili wa msanii  huyo kwa  kucheza nae.

Kutokana na polisi  kufanikiwa kumthibiti msanii  huyo na kumrudisha  jukwaani mashabiki walionyesha  kuchukizwa  kutokana na polisi kumtoa eneo hilo la mashabiki kiusalama na  kumrejesha  jukwaani  na  hivyo kuanza  kurusha  chupa za maji wakitaka  kumwachia  huru msanii  huyo awazungushie mauno. 

Wasanii  wengine  waliopagawisha  ni pamoja na msanii baba  Revo ,msanii Squza, msani Nyamidela  kutoka  Iringa ,msanii Jan Kihaga  wa Kihesa Iringa ambao  walionyesha  kuvutia  wengi katika uwanja  huo wa Samora  mjini Iringa
PICHA NA STORY KWA HISANI YA MATUKIO DAIMA

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname