HUYU NDIYE MODEL NA MUIGIZAJI WA KIKE ALIYE MJIA JUU NISHER BAADA YA KUJIFANANISHA NA ADAM JUMA..!!!
Zuhura Gora
Zuhura Gora ambaye ni model na actress nchini amemshukia Nisher ambaye
ni director na producer chipukizi wa video za muziki wa Bongofleva baada
ya kudaiwa kujilinganisha kiubora kwa kazi na Adam Juma ambaye alileta
mabadiliko ya kutengeneza video bora za muziki wa Bongofleva nchini.
Issue hiyo iliwafanya Nisher na Adam Juma waanze kutupiana maneno kwenye
mitandao ya kijamii na blogs kuanza kuandika habari hizo.
|
Zuhura Gora |
lakini Nisher ambaye pia
ana kazi nzuri licha ya uchanga wake kwenye fani hiyo alikaririwa na
Bongo5 akisema kuwa watu walimuelewa vibaya na wala hakumaanisha watu
walichotafsiri ingawa wengine walisema sio kweli anajibaraguza tu ila
alimaanisha hivyo hivyo.
Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Zuhura ambaye ni mpenzi wa Hemedy,
video model wa wimbo wa Kamili Gado wa Professor J na pia anatarajiwa
kuonekana kwenye tamthilia ya Siri Ya Mtungi season 2 aliandika " Hey
Nisher o vyovyotee unavyojiita stop kum-diss my boss coz humfikii hata
theluthii hujishtukiii kujifananisha na Adam Juma, nyooo mpxiiiieeww
jipangeee usiwe mburulaaa muoneee umeniboa for this haki ya Mungu walahi
umenitibua"
No comments:
Post a Comment