Diva wa muziki na muigizaji Zuwena Mohamed aka Shilole ambaye hivi sasa anafanya poa katika muziki Afrika Mashariki na kichupa chake kipya kiitwacho
'Nakomaa na Jiji' ameonyesha nia yake pia ya ushiriki wake katika tasnia ya filamu nchini Tanzania.
Akiongea na Paparazi wetu Shilole Kiuno au ukipenda kumwita Shishi baby amesema kuwa baada ya kumaliza kurekodi baadhi ya nyimbo zake zinazofuata ataingia rasmi katika uigizaji wa vichekesho 'Serious Comedy'.
Aidha Dashosti huyu anayewapagawisha mashabiki wake kwa kulimiliki vyema jukwaa katika show zake amesema kuwa mwaka 2013- 2014 ni mwaka wake wa kuonyesha kuwa yeye ni diva na amejipanga vilivyo kuliteka jiji kwa kishindo.
No comments:
Post a Comment