21 December 2013

SAMAHANI KWA PICHA YA KUTISHA...WIZI NI NOMA!! JARIBIO LA KUTAKA KUIBA PIKIPIKI AINA YA BAJAJI LAMSABABISHIA KIPIGO CHA PAKA MWIZI KIJANA HUYU EMBU TAZAMA HAPA!!


Mtu aliyetuhumiwa kujaribu kuiba pikipiki aina ya Bajaj maeneo ya Coco Beach Dar es Salaam akiwa tahabani baada ya kupata kipigo cha mbwa mwizi maeneo ya
Msasani jirani na Hospitali ya CCBRT hivi karibuni. Kwamujibu wa mashuhuda wa tukio hilo kijana huyo alikubwa na mkasa huo alipokuwa katika harakati za kukimbia na inadaiwa alikuwa na hirizi inayomsaidia kuendelea kupumua. Askari wa Kituo cha
polisi cha Oysterbay walifanikiwa kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala na tutawajuza kama anaendelea na hali gani. Kwa mujibu wa askari wa Kituo hicho wamethibitisha kumfikisha hospitalini na kwa kuwa hakuna anayemtuhumu baada ya kupata kipigo kikali watafanya mchakato wa kumlinda mpaka atoke hospitalini.







Wakazi wa Dar es Salaam wakimwangalia kijana aliyetuhumiwa kujaribu kuiba pikipiki aina ya Bajaj baada kupata kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira. Japokuwa kuchukua sheria mkononi ni uvunjaji wa sheria pia matukio ya mauaji ya jinsi hii yameendelea kutokea bila huruma kwa jamii ya Watanzania tofauti na miaka ya nyuma ambapo watu walikuwa na utamaduni wa kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ama kwa watendaji na haki kupatakana kwa watuhumiwa na wanaowatuhumu kuchukuliwa 
 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname