KITAULO cha kipa wa Simba, Ivo Mapunda ambacho mashabiki wa soka
Kenya wanakihusisha na imani za kishirikina kitaonekana leo Jumamosi
ndani ya Uwanja wa Taifa katika mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya
Yanga.
Ivo amesajiliwa na Simba akitokea Gor Mahia ya
Kenya ambayo ni watani wa jadi wa AFC Leopards pia ya Kenya. Kipa huyo
aliyesajiliwa na Simba kwenye dirisha dogo amekuwa maarufu Kenya
kutokana na kudaka penalti pamoja na kutundika kitaulo cheupe langoni.
Katika mechi za Gor Mahia na AFC kimekuwa kikiibua
utata baina ya wachezaji ambao hukihofia huku mashabiki wa timu yake
wakiamini kwamba kinawabeba na kumpa nguvu ya ushindi langoni.
Ivo alisema kwamba; “Hiki kitaulo ni cha kujifuta jasho tu wala hakina lolote.”
Mbali na AFC michezo mingine ambayo kitaulo hicho kiliibua utata ni dhidi ya Sofapaka na nyingine dhidi ya Tusker FC.
Tangu asajiliwe Simba mchezaji huyo wa zamani wa
Yanga atakuwa anaonekana kwa mara ya kwanza akiwa amevalia jezi ya Simba
kwenye mechi dhidi ya Yanga maarufu kama Mtani Jembe.
Mashabiki wamekuwa na hamasa ya kuona uimara wa
kipa huyo waliyekuwa wakimuona kwenye runinga pamoja na mbwembwe za
kitaulo chake ambacho hukitundika golini mechi inapoanza lakini baadaye
hukishusha kwa shinikizo la waamuzi
No comments:
Post a Comment