Denti huyo akiwa na mwanaye.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni jijini Mwanza akiwa hoi
kimaisha baada ya kufukuzwa kwa mwanaume huyo, denti huyo ambaye sasa
ana mtoto mwenye umri wa miezi saba, alisema baada ya kutoroshwa kwao,
mwanaume huyo alimpa mateso mengi, ikiwa ni pamoja na vipigo vya mara
kwa mara.
Mtuhumiwa aitwaye Roja.
Akisimulia kwa masikitiko, alidai kuwa Roja alimpa mimba akiwa bado
mwanafunzi wa kidato cha tatu mwaka 2012 na kumshawishi atoroke
nyumbani kwao ili akaishi naye.
Alidai kuwa, usiku wa Desemba 9 mwaka huu, Roja akiwa na baba,
alifika nyumbani na kumtaka aondoke mara moja huku akimtupia virago
vyake nje ya nyumba bila kujali kuwa na kitoto kichanga.
Hati ya makubalianao.
“Siku hiyo alifika nyumbani na kunitaka niondoke , nilipokataa
akaanza kunipiga na chuma kichwani na kunikaba shingoni bila kujali
nilikuwa na mtoto mgongoni. Nilipoona hali inazidi kuwa mbaya nikaamua
kuondoka zangu na kuja hapa ili nisaidiwe,” alisema mwanafunzi huyo
ambaye wakati huo alikuwa katika ofisi za taasisi inayojishughulisha na
utetezi wa haki za binadamu iitwayo Farijika.
Katika kuchimba ukweli wa madai hayo, Oparesheni Fichua Maovu (OFM)
ilizungumza na wazazi wa denti huyo ambao kwa muda tofauti walikiri
taarifa za mtoto wao kutoroshwa na kubakwa hadi kuzalishwa na mwanaume
huyo.
PF3.
Kuhusu manyanyaso anayopata mtoto wao, walisema anastahili matibabu
(PF3) ambapo vipimo vilionesha kuwa kweli alifanyiwa vitendo hivyo kwa
kuwa alikuwa na majeraha ya ndani kwa ndani.
Baada ya kuthibitisha hilo, Roja aliitwa mbele ya watetea haki hao na
kukiri kumnyanyasa mkewe lakini akiahidi kutomnyanyasa tena kabla ya
kusaini hati ya makubaliano iliyoshuhudiwa na mashahidi watatu, hati
ambayo kama akiivunja atafikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali
ikiwemo kubaka na shambulio la mwili.
Mama na mtoto wanaonyanyaswa na kijana Roja.
No comments:
Post a Comment