Tabu Ley Rochereau amefariki dunia leo asubuhi baada ya kulazwa hospitali kwa muda mrefu nchini Ubelgiji.
Akithibisha
taarifa za kifo cha baba yake kupitia radio Okapi, mwanae Charles Tabu
amesema mwanamuziki huyo aliyekuwa na umri wa miaka 73 amefariki
kutokana maradhi ya kisukari na kiharusi.
Naye
mwanamuziki mwenzake mkongwe Nyboma Mwandido, ameeleza kuwa marehemu
alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo tangu mwaka 2008 na kumfanya
ashindwe kusimama hadi mauti yalipomkuta leo asubuhi.
Tabu
Ley ni mwanamuziki ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali nchini
Congo ikiwa ni pamoja na kuteuliwa kuwa mbunge na Rais Raulent Kabila,
lakini pia aliwahi kuwa waziri wa Rais Raulent Kabila mwaka 1997.
Alizaliwa
November 13, 1940 na safari yake ya muziki ilianza rasmi mwaka 1954
aliporekodi wimbo wake wa kwanza ulioitwa ‘Bessama Muchacha’ akiwa na
African Jazz.
Katika
kipindi cha uhai wake ameweza kuwa moja kati ya wanamuziki wa Rhumba
waliokubalika zaidi duniani na hususani barani Afrika.
Apumzike kwa Amani
No comments:
Post a Comment