Wabunge wa nchini Uganda leo wameupitisha muswada wa
‘anti-pornography’ utakaopiga marufuku uvaaji miniskirts na nguo zingine
zinazotamanisha kimapenzi. Muswada huo unaopingwa vikali kama tishio
kwa haki za wanawake, unaweza kufanya filamu nyingi na tamthilia kupigwa
marufuku.
Wengine wanasema muswada huo unaweza kuzuia video nyingi za wasanii
kama Beyonce ama Rihanna kuchezwa kwenye runinga za nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor muswada huo unapiga marufuku
kitu chochote kinachoonesha sehemu za faragha kama matiti, mapaja na
makalio ama tabia yoyote inayoweza kuamsha hisia za mapenzi au tabia
yoyote inayoenda kinyume na maadili.
Muswada huo umekuja kufuatia kuongezeka kwa masuala ya pornography
nchini Uganda ni marudio ya kile kilichofanyika wakati wa uongozi wa Idi
Amin aliyepiga marufuku uvaaji wa sketi fupi miaka 1970s.
Leo pia wabunge wa nchi hiyo wamepitisha muswada wa kuzuia ushoga
nchini humo. Muswada huo unapendekeza kifungo cha maisha kwa mashoga au
kifo kwa wale wanaorudia makosa hayo. Kama muswada huo ukipita, mtu
yeyote atakayeshindwa kumripoti mtu anayejulikana kuwa shoga naye
anaweza kushtakiwa.
CREDIT-BONGO5
No comments:
Post a Comment