Msanii wa Hip Hop, Nay Wa Mitego usiku wa kuamkia leo ameibiwa vifaa
vya gari lake aina ya Toyota Verossa lenye namba T 418 CGK vyenye
thamani ya shilingi milioni 4 lililokuwa limeegeshwa nyumbani kwake.
Nay ameiambia Bongo5 kuwa jana aliliacha salama wakati anaenda kulala
lakini alivyoamka leo asubuhi,akakuta limenyofolewa baadhi ya vifaa.
Hizi ni picha za gari la Nay baada ya kuporwa baadhi ya vifaa vyake.
No comments:
Post a Comment