Msanii wa zamani wa kundi la Wakilisha, Witness Mwaijaga, amesema
pamoja na kufanya hip hop kwa sasa ni mfanyabiashara na mtaalam wa tiba
asili zinazotumia vyakula vyenye virutubisho.
Akizungumza na kipindi cha The Cruise cha East Africa Radio, Witness
alitoa ufafanuzi wa jinsi ulaji mbovu ulivyo na madhara kwa afya.
“Siku hizi watu wengi wamekuwa wanakula vyakula vyenye
cholesterol,kwa mfano mtu mwingine anaweza akawa na kansa au inaanza au
mwingine anaweza akawa ana high blood pressure,hajui tatizo ni nini.
Lakini mimi ninaweza nikakuelezea natural ukaelewa hiyo hali natural.
Kwasababu tu kula wengine mazoezi,at the same time. Wakati mwingine kuna
tatizo lingine ambalo tunalo hapa obesity, suala la ‘unene’ huku kwetu
ndio kabisa kwasababu hata mafuta tunayotumia na vyakula vingi viko
namna hiyo, watu wanakula nyama nyama sana na vyakula vingi vyenye
cholesterol,” alisema rapper huyo.
Kwa upande wa muziki, rapper huyo amesema amemaliza kurekodi video
mbili, moja inaitwa ‘Nadata Nawe’ na nyingine inaitwa ‘Think About’
ambazo zote zitatoka mwakani.
No comments:
Post a Comment