Msajili wa Vyama vya Siasa,Jaji Francis Mutungi
Ofisi
ya Msajili wa vyama vya siasa nchini, imethibitisha kupokea barua ya
aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema )
mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Akizungumza
na paparazi wetu kwa njia ya simu, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji
Francis Mutungi, alithibitisha kupokea barua hiyo na kueleza kuwa ofisi
yake inaifanyiakazi.
“Tumepokea barua ya Mwigamba,
lakini siwezi kueleza kilichomo ndani yake kwa kuwa ndiyo tunaifanyia
kazi…tutawaita wanahabari kuwaeleza hatua zilizochukuliwa na ofisi
yangu,” alisema Jaji Mutungi.
Hivi karibuni katika mkutano
na waandishi wa habari, Mwigamba ambaye amevuliwa madaraka yake yote
ndani ya chama na wenzake, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na
Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo, aliwasilisha malalamiko yake
kwa msajili.
Katika taarifa yake Mwigamba,
amemuomba msajili kutoa mwongozo kuhusu anachodai kuwa ni mgogoro wa
kikatiba uliopo ndani ya Chama kufuatia kipengele cha katiba
kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume na utaratibu.
“Katiba ya Chadema ya mwaka
2004 kipengele 5.3.2 (c) inasomeka ifuatavyo kuhusu Muda wa
Uongozi:Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea na
kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa
kiongozi kwa muda usiozidi vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi
moja,” alidai Mwigamba.
“Sentensi kuhusu ukomo wa
uongozi haipo. Ni kweli kuwa Marekebisho ya Katiba yalifanyika mwaka
2006, lakini hoja ya kubadili kipengele hicho haikuwepo na muhtasari
zinaonyesha wazi kuwa kulikuwa hakuna mjadala wa kipengele hicho au
kuhusu suala zima la ukomo wa uongozi,” anadai.
Novemba 22, mwaka huu, Kamati
Kuu iliwavua madaraka viongozi hao na kuwataka wajieleze kwa maandishi
ndani ya siku 14 baada ya kudaiwa kuhujumu chama kwa kuandika waraka wa
siri unaodaiwa pamoja na mambo mengine, kuwadhalilisha viongozi wakuu wa
Chadema.
No comments:
Post a Comment