Naona siku hizi habari nyingi ambazo mastaa hutaka ziwe siri, zinavuja
kirahisi pale wanapokwenda kujirusha sehemu sehemu au wakati mwingine
ushahidi watu wanautengenezea kutoka kwenye mitandao ya kijamii kama huu
wa Instagram ambao ni maalum kwa kupost picha mbalimbali.
Baada ya utangulizi huo basi, naomba kukupa moja ya taarifa kubwa
kwenye mitandao ya Nigeria kwamba mwimbaji D’Banj ameripotiwa kwamba
yuko mapenzini na mrembo Yaris Sanchez raia wa Dominican Republic, nchi
yenye watu zaidi ya milioni 10 kwa mujibu wa takwimu za WB 2012.
Unaambiwa
Mnigeria D’Banj na Yaris walichukua ndege private mpaka sehemu inaitwa
Asaba huko Nigeria kwa ajili ya kwenda kula bata ambapo mrembo huyo
aliamua kupost pichaz akiwa kwenye hizo bata za Nigeria.
Mpaka
sasa, mrembo huyu ambae ni mama wa mtoto mmoja ameshatajwa kwenye
headlines za kuwa mapenzini na mastaa wa dunia kama Fabolous, Sean
Kingston, Lloyd Banks, Joe Budden na Bobby Valentino.
Yaris na rapper Joe Budden wakati wa mapenzi yao..
Hizi picha mbili za juu ni wakati Yaris alipokua Nigeria.
No comments:
Post a Comment