Staa wa sinema na muziki Bongo, Snura Anton Mushi na Kiungo
Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa wamenaswa ‘laivu’ wakiwa
kimahaba,
Ngassa akiwa kimahaba na Snura.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, tukio hilo lililijiri hivi karibuni
nyumbani kwa Snura maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambapo
wawili hao walibambwa wakiwa wamejiachia ‘wakifanya yao’.
Mnyetishaji huyo alidai kuwa wawili hao walikuwa wakiminyana bila kujali macho ya watu waliokuwa wakifika nyumbani kwa Snura hasa marafiki na majirani zake.
Mnyetishaji huyo alidai kuwa wawili hao walikuwa wakiminyana bila kujali macho ya watu waliokuwa wakifika nyumbani kwa Snura hasa marafiki na majirani zake.
“Yaani walikuwa wakioneshana mahaba kama njiwa bila kificho chochote.
“Kuna ‘taimu’ Snura alikuwa akimpakata Ngassa utadhani mtoto mdogo.
“Baadaye hata Ngassa naye alifanya hivyohivyo huku akicheza na nywele za Snura anavyotaka,” alidai shuhuda wetu.
“Kuna ‘taimu’ Snura alikuwa akimpakata Ngassa utadhani mtoto mdogo.
“Baadaye hata Ngassa naye alifanya hivyohivyo huku akicheza na nywele za Snura anavyotaka,” alidai shuhuda wetu.
Ili kujiridhisha, Amani lilisaka picha za wawili hao ambazo walikuwa
‘wakijifotoa’ kwa simu zikiwaonesha wakiwa katika mahaba jambo lililozua
utata na maswali kwa walioziona.
...Wakiwa katika pozi.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibainisha kuwa siyo mara ya kwanza kwa
Snura na Ngassa kunaswa wakiwa beneti kwani wiki mbili zilizopita
walibambwa kwenye ukumbi mmoja wa starehe jijini Dar wakila bata ndefu.
Baada ya kulishwa ‘niuzi’ hizo, gazeti hili lilimsaka Snura ambapo
alipopatikana alitakiwa alimwagiwa habari yote juu ya uhusiano wake tata
na Ngassa ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nimeshtuka sana kusikia hizo picha zimewafikia kwa sababu mimi na
Ngassa ni marafiki na yeye (Ngassa) ni shabiki mkubwa wa nyimbo zangu.
“Ngassa alinitembelea kama marafiki wengine wanaokuja nyumbani
kwangu. Simu yangu ilipotea ndiyo maana picha zikavuja lakini ukweli
ndiyo huo.”
...Wakizidi kujiachia kimahaba.
Kwa upande wake Ngassa ambaye yupo mapumzikoni baada ya kumalizika
kwa msimu wa kwanza wa Ligi Kuu Bara hakuweza kusema chochote kufuatia
simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.
Chanzo: GPL
No comments:
Post a Comment