Waandishi
wengi walikua na maswali mengi kuhusu yeye kusimamishwa kuwa Mwenyekiti
wa Simba lakini akayapangua kwa kusema kesho mchana ndio atazungumza na
Waandishi kuhusu kila kitu ila sentensi moja iliyonyakwa na
millardayo.com ni ‘taarifa za kusimamishwa Uwenyekiti sijazipata ndio
kwanza nakusikia wewe, ninachojua mimi bado ni Mwenyekiti wa Club ya
Simba’
‘Nimefurahi
kwa mapokezi mazuri ambayo yameonyesha imani ya Wanachama kwangu mimi,
mimi kama Mwenyekiti nitatoa tamko langu rasmi kesho mchana makao makuu
ya Club ya Simba, sasa hivi siwezi manake rafiki yangu mpenzi Zitto
kabwe ameondolewa kwenye Unaibu katibu mkuu na mimi sijafurahia kwa hiyo
siko kwenye mood ya kuongea’ – Aden Rage
Alipoulizwa
kama ana taarifa za kocha mpya Simba na pia kikao hicho atakifanyiaje
Makao Makuu wakati ameondolewa kwenye Uwenyekiti, Rage kasema swala la
kocha atalizungumza kesho ila hilo la kufanyia mkutano na Waandishi wa
habari makao makuu ya Simba, waandishi wasiwe na wasiwasi kwani yeye
ndio Mwenyekiti.
No comments:
Post a Comment