Marehemu Hamida Urembo
Ni kifo cha
kusikikisha cha mwanamke huyo pichani Hamida Urembo na muhusika wa
mauaji hayo ni mumewe wa ndoa waliyeishi kwa miaka mitatu.Hamida alikuwa
mwanafunzi wa chuo kikuu na mwaka watatu na alikuwa anatarajia
kugraduate mwezi huu chuoni hapo.
Hamida na
mumewe yahaya walibahatika kupata mtoto wa kike mwenye miaka mitatu
sasa.Kwa mujibu wa dada wa Hamida ndoa yao ilikuwa ya misuko suko
sana.Mume alikuwa sio mwaminifu mara nyingi alikuwa akizini nje.Ukiacha
hilo alikuwa akimpiga sana mkewe mpaka kumzimisha.
Matatizo
ambayo ndugu walikuwa wakiyajua na walishasuluhisha mara nyingi na
Hamida kurudi kwa mume kuendelea na maisha.Hii ya mwisho ndio ilikuwa
kubwa zaidi.Mume alikuwa akimtongoza housegirl hapo nyumbani na
alipokuwa kesho housegirl akamfahamisha mama.
Akamueleza
jinsi gani muwewe amekuwa akimsumbua kumtaka kimapenzi.Hamida akamwambia
anataka tu uthibitisho kama ni kweli.Siku ya siku Yahaya akamlazimisha
Hamida kwenda kwao na Hamida akakubali akijua kuna jambo.Akasindikizana
na mumewe mpaka kituoni mume akijua mkewe hayupo kumbe mke aligeuzia
njiani akarudi nyumbani akajificha chini ya uvungu chumbani kwa
housegirl wake.Baadae mume akawasilia na housegirl kuwa anarudi
nyumbani,aliporudi akaendelea kuomba mambo tena akavua nguo kabisa
akabaki na boxer.Wakati huo yupo chumbani kwao na mkewe.Housegirl
akamwambia wahamie chumbani kwako hapo sio salama.Basi wakahamia
chumbani na akawa ndio anamuinamisha dada ili amfanye Hamida akatoka
chini ya uvungu ili kumuokoa dada na kumuonyesha mumewe kuwa alikuwepo
na amejua usaliti wake.Na alipokuwa chini ya uvungu alikuwa akirekodi
kila kitu kwenye simu na alipotoka na picha akapiga.
Huyu ndiye Yahaya aliyekuwa mume wa marehemu Hamida |
Hamida alitoka
hapo akashitaki kwao na kwao wakamwambia aende kwa mjomba wa mumewe
kumueleza matatizo ya mtoto wao. Alipofika kwa mjomba akaambiwa wanaume
ndivyo walivyo avumilie tu arudi kwa mumewe.
Hamida
akarudii kwao akiwa hana hana raha lakini uamuzi aliouchukua ni
kuachana na mumewe kwani alikuwa kashachoka. Wakawa wakivutana sana mume
akimsihi arudi nyumbani walikokuwa wakiishi Mbagala ila Hamida
hakuridhia.
Hamida alishaenda mpaka Bakwata ili mumewe aamriwe kutoa talaka.
Mwisho wa
Hamida kuonekana nyumbani ni siku ambayo yeye na ndugu zake walikuwa
waende kijijini kwao kwenye viwanja walivyopewa na babu yao.Ila siku
hiyo Hamida alitoa udhuru kuwa haendi na akamtaarifu mama yake kuwa
Yahaya kamuita akachukue vitu vyake vilivyobakia.Mama akamkatalia kwenda
akamwambia kuna kaka zake wakubwa aache wataenda kuvifata kwani huyo
mume ni mshenzi anaweza kumfanyia kitu kibaya.Hamida akamwambia mama
anataka kwenda mwenyewe kwani kuna vyeti vyake muhimu akavichukue.
Basi mama
akamuacha aende kishingo upande lakini mama akamwambia basi nenda hata
na mdogo wako.Akaenda na mdogo wake lakini kufika kule mume akamkatalia
mdogo mtu kuingia ndani.
Wakabishana
sana kwa nini asiingie mdogo mtu kuepusha shari akaenda kukaa kwa jirani
asubiri kuitwa. Akakaa na muda kupita kukawa kimya akajua wale
wameelewana ndio maana hakuna makelele hivyo akaendelea kusubiri.
Akakaa weee
mpaka jioni giza lilipoanza kuingia kidogo Yahaya akampigia simu kwa
kutumia simu ya Hamida akimwambia aondoke tu arudi nyumbani wao
wameshaondoka na vyombo wamebeba.
Mdogo mtu akaondoka kurudi nyumbani kwao Tabata akijua mke na mume wameelewana kumbe dada yake ameshakufa ndani.
Mdogo mtu
akafika nyumbani saa mbili usiku na kumwambia mama jinsi Hamida
alivyomuudhi kamuacha yeye kwa jirani na akaondoka na mumewe Yahaya.Mama
machale yakamcheza akanyanyua simu akampigia Yahaya kumuuliza mwane
yupo wapi.Yahaya akamjibu kuwa ameachana nae kitambo mama akamwambia sio
kweli mwanangu hawezi kuchelewa kurudi nyumbani na hana kawaida
hiyo.Yahaya akamjibu atarudi tu Hamida mtu mzima.
Mamam tayari
alishajua kuna jambo akampigia simu baba Hamida aliyekuwa Arusha
kumtaarifu kilichotokea. Baba Hamida akampigia Yahaya lakini hakupokea
simu.Wasiwasi ukazidi kutanda na ndugu kupeana taarifa zaidi.Asubuhi
kulipokucha wakaenda Mbagala kwa Yahaya lakini wakatoa taarifa
polisi.Polisi wakawaondoa wasiwasi kwamba hao wanajuana wenyewe labda
wameamua kukumbushiana.
Ndugu
hawakuridhika wakaenda kwa mjumbe awaruhusu wavunje nyumba waingie ndani
pengine kamfungia ndani maana ilikuwa kawaida yake kufanya hivyo
kumfungia Hamida ndani.Basi mjumbe akaruhusu mlango uvunjwe walipoingia
ndani palikuwa patupu hawakuona kitu wala dalili za mauaji.Kuna chumba
ambacho ni stoo hicho walishindwa kufungua na mjumbe akawaambia hiyo ni
stoo wanawekaga mavitu yamejazana humo basi wakakiacha wakaondoka.
Hawakuishia hapo bado waliendelea kumsaka Hamida bila mafanikio.
Hamida
alipotea toka jumapili iliyopita,jumanne juzi kila mtu wakapanga kila
mtu akamtafute popote pale anapoona anaweza kumpata.Mama akaenda kwenye
maombi kanisani wakati muislam,dada akaenda blue pearl kazini kwa Yahaya
na huku majirani Mbagala wakaanza kuona inzi na harufu kali ikitoka
nyumbani kwa Yahaya.Ikabidi mjumbe apige simu kwa mama Hamida kumueleza
kinachoendelea polisi wakaitwa,nyumba ikavunjwa ili kutafuta harufu
inatokea wapi.Wakavunja kile chumba cha stoo na kukuta mwili wa Hamida
umeshaanza kuharibika.Kanyongwa na kamba ya katani na kitenge kafungwa
puani na mdomoni.Mwili wake ukawekwa kwenye mfuko akajaziwa mito na
manguo nguo na tendegu la kitanda kawekewa shingoni.
Ndugu, polisi wakachukuwa mwili kwa ajili ya msiba na mazishi wakati huo Yahaya alishakimbia siku nyingi hajulikani alipo.
Hamida
alizikwa jana kule kwa babu yake Mzenga uzaramuni walipokuwa
waende kwenye mashamba waliyopewa. Msiba upo nyumbani kwao Tabata.
Mrehemu ameacha mtoto wa kike wa miaka mitatu anaitwa Tayana.
Habari hii inaendelea tena kesho katika heka heka za leo ndani ya leo tena ya clouds fm.
R.I.P Hamida na tunatoa pole kwa familia nzima ya Urembo kwa msiba
No comments:
Post a Comment