Shoo ninayoweza kufanya kwa bei ya chini kabisa
ni Sh 10 milioni za Kitanzania na hii labda nione anayeniomba nifanye
shoo hiyo hayuko vizuri na pengine ni rafiki yangu na hawezi kuninyonya,
si hivyo tu itategemea pia ni kampuni gani na ni watu wa aina gani
ambao watanitaka nifanye nao kazi.
UKIFIKA katika mtaa anaoishi mwanamuziki Diamond
maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam utaanza kuhisi kuwa kuna staa
anayeishi maeneo hayo, macho ya wengi huanza kumtazama mtu anayeelekea
katika geti la nyumba anayoishi msanii huyo.
Muda wote geti hilo limefungwa. Ili uweze kuingia
ndani itakulazimu ubonyeze kengele itakayoashiria kuwa kuna mgeni nje
anahitaji kuingia ndani. Hata hivyo hauwezi kupenya kirahisi ndani hadi
uulizwe shida yako na kama hauna miadi na mtu yeyote anayeishi ndani ya
nyumba hiyo haitakuwa rahisi kuingia.
Mwanaspoti lilitinga
katika nyumba ya msanii huyo na kushuhudia ukimya wa hali ya juu ilhali
kuna watu ndani. Baada ya kufunguliwa geti tuliingia ndani na kupokewa
na Diamond aliyekuwa ameketi katika sebule iliyonakshiwa na mapambo
makini ukutani huku ikiwa na samani chache lakini za gharama kubwa.
Tulitumia saa mbili mfululizo katika mahojiano na
Diamond ambaye alifunguka kwa kila swali aliloulizwa na kujibu kwa
ufasaha na ufafanuzi mpana.
Mwanaspoti: Utendaji kazi wako ukoje katika muziki?
Diamond: Nina mipango makini katika kazi zangu.
Mambo yote lazima yapitie kwa meneja wangu ndipo yanifikie mimi, mara
nyingi mtu hawezi kuzungumza na mimi moja kwa moja lazima apite huko na
hiyo ndiyo staili ya Diamond. Nimejipanga kuhakikisha nafanya kazi gani,
kwa wakati gani na sikurupuki tu, japo katika utengenezaji wa nyimbo
zangu naweza nikapata wazo basi hapo hapo nikatengeneza mistari.
Mwanaspoti: Utendaji kazi wako ukoje kuanzia asubuhi hadi jioni?
Diamond: Saa tano asubuhi, nikishaamka kitu cha
kwanza ni kwenda ‘gym’, mara nyingi ni hapa nyumbani kama unavyoona hapo
nje kuna sehemu ya mazoezi na sehemu nyingine zilizopo ndani, mara
nyingi hutumia muda wa saa moja. Ifikapo saa sita na nusu huwa naanza
kufanya kazi zangu lakini itategemea na ratiba zangu za siku ambazo ndio
mwongozo wangu wa kuimaliza siku. Baada ya hapo napumzika kwa muda
fulani na baadaye jioni huendelea na kazi na mara nyingi kazi zangu huwa
nazimaliza usiku wa manane.
Mwanaspoti: Unalala saa ngapi? Na unalala kwa muda gani?
Diamond: Muda wangu wa kulala
mara nyingi ni saa kumi na moja alfajiri na kama sikuwa na kazi nyingi
studio basi nitalala saa nane usiku. Muda wangu wa kulala ni saa sita
mpaka nane kwa siku. Ila hata kama nikilala mapema kuamka ni saa tano
asubuhi ila itategemea na nini ninakifanya siku inayofuata na kama nina
kazi maalumu na ya mapema itanilazimu niamke mapema ili kuzikamilisha.
Mwanaspoti: Shughuli gani zinazokuchelewesha mara kwa mara kulala?
Diamond: Ni kurekodi na wakati
mwingine shoo. Kwa wiki ninafanya shoo nyingi, kama ni tatu basi siku
zote tatu nitalala alfajiri. Siku nyingine zinazosalia ninalala usiku wa
manane kwa kuwa huwa nakuwa studio na sehemu nyingine ambazo hunilazimu
kufanya kazi kwa kipindi kirefu usiku
No comments:
Post a Comment