Kipindi
cha TV cha Bongo Dar es Salaam ambapo ndani yake huigiza Dude,
kilizuiliwa kuoneshwa kwenye TV na polisi waliodai kuwa kinafundisha
watu kuwa matapeli, imebainika.
Taarifa hiyo imetolewa na mwanzilishi na mmiliki wa kipindi hicho kilichokuwa kikioneshwa TBC1, Mrisho Mpoto.
“Ilifika
wakati polisi walitutumia barua na wakisema kuwa ‘kwanini Dude
Hakamatwi? Kila siku tunamuona anawatoka polisi,tunataka hkamatwe
kwasababu mnalidhalilisha jeshi la polisi kama limeshindwa kufanya
kazi’.Huku wengine wakisema tunafundisha watu mbinu za utapeli,wengine
wakisema kipindi kizuri na kinaelimIsha watu ambao wanaingia Dar es
Salaam. Basi kwasababu walitupiga stop tukaona ngoja tutafute mbinu
nyingine,” Mrisho ameiambia Bongo5.
Katika
hatua nyingine, Mpoto amesema kwasasa hawezi kukiendesha tena kipindi
hicho na hivyo atamuachia mikoba Dude, ambaye ni muigizaji mkuu. Amesema
sasa hivi anajishughulisha na mambo ya muziki na pamoja na kuendesha
makampuni yake yanayomwingizia fedha nyingi zaidi.
“Kipindi
cha Bongo Dar es salaam ni cha kwangu. Mimi ndio producer na Dude
alikuwa kama partner, kwasababu alikuwa ni mhusika mkuu. Kwahiyo hata
kama nikaamua kukirudisha naweza nikaenda kurenew kibali nikaendelea
kuproduce kwasababu mimi ndio nimekisajili,” amesema Mpoto.
Mpoto
amesema alisikia taarIfa kuwa Dude alitaka kwenda kukiuza kipindi hicho
M-Net bila kumtaarifu lakini aligonga mwamba kwakuwa hati za umiliki
walizozihitaji anazo yeye.
“Namwachia
Dude kiwe cha kwake kwasababu yeye ni mwigizaji na mimi nafanya
shughuli tofauti na hizo. Ingawa makaratasi ya usajili yote ninayo kama
akiyahitaji nitampatia kwasababu nimesikia kwamba anashindwa kufanya
mambo ya kukiendeleza kipindi kwasababu hana hati ya umiliki wa kipindi.
Ili ni tatizo la Watanzania wengi kushindwa kusema ukweli wa mambo.
Nasikia Dude alienda, M-Net kwenda kuuza vipindi,ila ikashindika
kwasababu walihitaji document za umiliki na document zote ninazo mimi.”
Imeandikwa na: BONGO5.com
No comments:
Post a Comment