10 November 2013

ALLY CHOKI ANUNUA GARI JIPYA LA TSH.MILION 52 KULINDA HESHIMA


Stori: Shakoor Jongo
ILI kulinda heshima ya ukurugenzi, Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki amevuta mkoko Toyota Prado yenye thamani ya shilingi milioni 52.

Mkoko mpya wa Ally Choki aina ya Toyota Prado ofisi za GPL.
Choki amenaswa na ndinga hiyo juzikati jijini Dar ambapo paparazi wetu alipomuuliza sababu za kuongeza ndinga hiyo ilihali ana magari mengine likiwemo Toyota Noah, Choki alitaja kigezo cha heshima kuwa sababu iliyomfanya anunune ndinga hiyo.
Muonekano wa mbele wa Toyota Prado.
“Unajua kila kitu kinakwenda na mipango lakini wakati mwingine heshima ya mtu inajengwa na vitu vidogovidogo hivyo niliona angalau ndinga kama hii inaendana na mimi, siyo kwamba nimenunua kuonesha jeuri, hapana lakini heshima nayo inahusika barabarani,” alisema Choki.
Kuhusu suala la kujipendelea kununua magari yeye kama mkurugenzi, Choki alisema yeye na bendi yake huwa hawana matatizo ya magari ya kusafiria ndiyo maana wana magari zaidi ya saba yanayotumika kwa shughuli za bendi.
Choki kama mkurugenzi na muimbaji, anakuwa mwanamuziki wa kwanza kumiliki gari la thamani katika wanamuziki wa dansi Bongo

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname