Katika hali isiyotarajiwa katika wasanii wanaounda
kundi la Bongo Movie ambalo linaundwa na baadhi ya wasanii wa filamu Swahiliwood
wamejikuta wakijitenga kushiriki msiba wa baba mzazi wa msanii mwenzao Wema
Isack Sepetu, baada ya kuundwa zengwe na mmoja wa watu wenye ushawishi katika
kundi hilo, Wema akiongea kwa huzuni amesema kuwa hata wale waliofika jana
katika msiba huo hawakufika kwa ajili ya kumfariji bali walifika kwa ajili ya
kumsanifu.
filamucentral.co.tz ilifanya utafiti ili kubaini hilo
kwa kuwapigia simu baadhi ya wasanii wanaotoka katika kundi hilo nao bila kusita
kwa masharti ya kutotajwa majina walitiririka kwa kusema kuwa ni kweli uongozi
wa kundi hilo umetoa agizo watu wasishiriki kutokana na tabia ya msanii huyo
kutoshiriki katika misiba ya wasanii wenzake.
“Ni kweli hilo lipo na
lina ukweli kwa njia moja au nyingine Wema bwana huwa hashiriki katika misiba ya
wasanii wenzake, kuna mtu muhimu sana na ana sauti katika kundi la Bongo Movie
amesema kuwa katika misiba iliyotokea ameshiriki misiba miwili tu, wa marehemu
Sharo na Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake,”anasema kijana
huyo.
Hili si jambo la kulifurahia kwa wasanii kwani halijengi bali
linaleta mgawanyiko wa moja kwa moja, msanii mwingine alikiri kuwa Wema anabagua
kushiriki misiba kwani wakati amefariki marehemu John Maganga alipigiwa simu ili
ashiriki katika msiba lakini alisema yupo Location, hivyo wasanii wenzake
wanamtenga ili aone umuhimu wa kushiriki misiba ya
wenzake.
Jana jioni nyumbani hakukuwa na wasanii zaidi ya
mtangazaji wa kipindi cha Take One Zamaradi Mketema akiwa na Rais wa shirikisho
la wasanii Simon Mwakifwamba na waombolezaji wengine, huku baadhi ya wasanii
wakifika pale na kuondoka jambo ambalo Wema alilitafsiri kama walifika pale
kutoa lawama ili asiwaone kama hawajafika lakini hawakuwa na dhamira ya kweli
mioyoni mwao.
unapo copy story kutoka blog za watu weka credt zao kuonyesha kumkubali na kuheshimu kazi ya mtu usiwe mwepesi kucopy tu haipendezi bwana itafika kipindi watu wata block blog zao iwe huwezi ku copy na si poa toa credt kwa aliyeandika hii sio kwako tutahakikisha tunaziumbua blog kama yako ambayo ni wepes ku copy ila hamtoi credt mfano habar hiyo ya wema ume copy thesuperstarstz hata kumpa creadt umeshindwa acha hizo ww ni mimi muumbuaji na msema kweli siku zote
ReplyDeletempekuzi! kwani uongo
Delete