30 October 2013

BAADA YA KUAMBIWA ILE GARI ALIYOONYESHA IRENE UWOYA JANA AMEHONGWA NA MAPEDESHEE..!! UWOYA AFUNGUKA NA KUSEMA....!!



0713472e3e5211e396f322000ae908d3_8
 Baada ya fans wengi kuanza “kumponda” mwanadada Irene Uwoya kuwa gari aina ya Range Rover aliyoinunua “amehongwa na washika dau”, mwanadada huyo ameibuka na  kusema kuwa mali anazomiliki amezinunua kwa pesa zake anazopata kwenye uigizaji  pamoja na zile zinazotokana na biashara zake nyingine. 3acbe8643e5211e3838722000ae910b6_8  
“Kwa nini watu hawataki kukubali kuwa kazi ya uigizaji inalipa, yaani sisi tukinunua magari tumehongwa? Yaani wa kuhongwa ni sisi tu na si tasnia nyingine?” alihoji Uwoya. aecd0b023e6211e39bf922000ab5b971_8 7fe5658c3e6211e3b45022000a1fb3cd_8 Aidha Uwoya alisema kuwa kazi ya filamu ukijua kuitumia vizuri kwa kujiwekea malengo na kuitumia vizuri kila senti unayoipata, unaweza kupata mafanikio makubwa. “Tunaigiza sehemu nyingine ambazo hutaki hata mwanao aone, hii siyo kazi rahisi maana yake ni kwamba kama ukiipatia unaweza kujikuta unaingiza pesa kila siku kwani mwaka mzima uko kazini,” alisema Irene amesema kuwa ameamua kuweka wazi ukweli huo kutokana na maneno yaliyozagaa kuwa magari anayomiliki amenunuliwa na wanaume ‘wanaomweka mjini’.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname